Divisheni ya fedha na deni la Taifa inashughulika na udhibiti na usimamizi wa deni la Taifa.
Majukumu ya Divisheni ya Fedha na Deni la Taifa
- Kusimamia Deni la Taifa kwa kuandaa muundo wa usimamizi wa deni na kuhakikisha mzigo wa madeni unadhibitiwa.
- Kutathmini mapendekezo ya mikopo ya ndani na nje na kuandaa usimamizi wa kujitegemea katika wajibu wa kifedha wa Serikali.
- Kudumisha “database” ya usimamizi wa madeni ya mikopo na dhamana ya Serikali.
- Kuandaa ripoti za madeni kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma.
- Kusawazisha taarifa za madeni ya Serikali na wanaotudai, BOT, Wizara ya Fedha na Mipango, SMT na wadau wengineo.
- Kukusanya, kuhakiki na kutoa taarifa ya madeni yote ya ndani ya Serikali.
- Kutayarisha makisio ya riba ya Deni la Umma na malipo ya Kima kwa ajili ya kuiingiza katika bajeti ya mwanzo.
- Kutimiza matakwa ya Serikali kifedha na kuweka gharama ndogo na madeni kadiri iwezekavo zinazohusiana na vihatarishi.
- Kutunza kumbukumbu za Madeni ya Serikali na kufuatilia mfumo wa Usimamizi wa madeni.
- Kutoa dhamana na kuweka kumbukumbu za malipo ya dharura kwa Taasisi za Umma, mashirika na Serikali za mitaa.
- Kutoa taarifa za mwenendo wa Fedha katika Mfuko Mkuu, malipo ya deni na salio la mtawanyo wa mkopo.
- Kutoa kazi za sekriterieti ya Kamati ya Usimamizi wa Deni la Zanzibar.