Kitengo hiki kitahusika na masuala ya mahusiano kati ya Ofisi na taasisi nyengine, kuratibu malalamiko na kuzitangaza shughuli za Ofisi Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.
Majukumu ya Kitengo.
- Kupokea maoni na hoja za wananchi, kuzifuatilia na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kwa lengo la kufanyiwa kazi.
- Kukuza na kujenga uhusiano mwema kati ya Ofisi ya Rais Fedha na Mipango na Taasisi nyengine;
- Kupokea malalamiko kutoka kwa wadau juu ya utendaji wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
- Kufuatilia maendeleo na changamoto za mahusiano kwa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
- Kuweka mazingira mazuri na kukuza mahusiano kazini baina ya watumishi wa Ofisi, watumishi wa Taasisi nyengine na jamii kwa ujumla (afya, michezo, usalama na utamaduni);
- Kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ya kiitifaki ya Ofisi;
- Kuratibu na kupokea wageni wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.