Divisheni hii imeanzishwa kwa lengo la kukuza sera za kodi na kuchambua athari za sera kodi kwenye uchumi na kuhakvishikisha mifumo ya kodi inakuwa bora, yenye ufanisi, usawa, haki na rahisi kueleweka na kutekelezeka.

majukumu ya divisheni ya sera za kodi

  1. Ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wake na pia kukadiria athari za mapato kutokana na mikakati ya hatua mbalimbali za kuimarisha mapato na kuhakikisha hali nzuri na imara ya kodi ndani ya uchumi.
  2. Kufuatilia na kushauri Serikali juu ya usimamizi wa mapato yatokanayo na Kodi na mapato yasiyokuwa ya kodi kwa Taasisi zinakusanya mapato na kupendekeza hatua za kukabiliana na hatua za kukwepa kodi na ukwepaji wa kodi.
  3. Kufanya uchambuzi wa mapato na kufanya makadirio ya mapato yatokanayo na kodi na yasiyokuwa ya kodi katika kuhakikisha utulivu wa sera za kodi na matumizi.
  4. Kushauri Serikali juu ya Ugawanyaji wa Fedha pamoja na uhusiano kati ya Serikali kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
  5. Kushauri Serikali juu ya muundo, utekelezaji na usimamizi wa matumizi mabaya ya misamaha ya kodi (misamaha ya kodi na Unafuu wa Kodi) kufikia malengo ya kisera kwa maendeleo ya uchumi.
  6. Kushauri Serikali juu ya sheria za kifedha za kuaminika (kama sheria za deni na sheria za matumizi), pamoja na uchambuzi wa uendelevu wa deni, kudhibiti kukopa na kuhakikisha kuwa serikali inaweza kulipa deni lake wakati wowote kutokana na mapato.
  7. Kushiriki na kuishauri Serikali katika ujumuishaji wa kikanda kama vile EAC, SADC, COMESA kwenye maswala ya Sera za Kodi.
  8.  Kushauri Serikali katika kuandaa mfumo wa Sera ya mkataba wa kodi na mkataba wa mfano na kushiriki mazungumzo ya makubaliano ya utozaji wa Kodi ya mapato (Mikataba ya kuondoa utozaji kodi mara mbili).
  9. Kushauri juu ya matumizi ya sheria za kodi kwa miamala na biashara za kimataifa.