Divisheni ya utekelezaji na ufuatiliaji wa bajeti inashughulika na kusimamia upatikanaji wa taarifa sahihi za mapato na matumizi ya Serikali.
Majukumu ya Divisheni ya Utekelezaji na Ufuatiliaji wa Bajeti
- Kusimamia taarifa za Mapato na matumizi halisi za Mawizara na Taasisi;
- Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya robo mwaka, nusu mwaka na ya mwaka;
- Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali;
- Kubuni mpango kazi na mpango wa maombi ya fedha kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
- Kusimamia uingizwaji wa fedha ndani ya mfumo mjumuwiko wa fedha (IFMS);
- Kusimamia matumizi kwa kila robo mwaka na kuiwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
- Kuratibu utekelezaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Ofisi ya Mhasibu Mkuu/ Hazina, Idara ya fedha za nje na Tume ya Mipango;
- Kubuni mipango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni nyengine;
- Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.