Divisheni hii inashughulika na uhifadhi na udhibiti wa taarifa za mishahara.
Majukumu Divisheni ya Uhifadhi na Udhibiti Taarifa za Mishahara
- Kubunia njia bora za usimamizi ripoti za mishahara (CPO) Kwa ajili ya matayarisho ya malipo;
- Kuratibu uchapishaji wa taarifa za mshahara kwa kila mfanyakazi;
- Kusimamia uandaaji MTEF na mpango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni;
- kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka
- Kuratibu marekebisho yaliyoidhinishwa ya wafanyakazi ndani ya Database ya mishahara;
- Kubuni njia bora ya uwasilishaji wa taarifa za mishahara kwa kila mwezi kwa Taasisi husika za Serikali;
- Kubuni mageuzi yoyote yanayoigusa bajeti ya Serikali.