Divisheni hii inashughulika na uandaaji wa bajeti kwa kuingizwa taarifa za bajeti kwenye mfumo wa kielektronik.
Majukumu ya Divisheni ya Uandaaji Bajeti
- Kuratibu uwasilishwaji wa bajeti za Mawizara na kusimamia uingizwaji wa taarifa za bajeti kwenye mfumo wa kielectroniki;
- Kusimamia uchapishaji wa hutuba ya bajeti ya Serikali pamoja na makadirio ya Mapato na matumizi;
- Kuratibu mswada wa fedha na matumizi;
- Kuratibu utekelezaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Ofisi ya Mhasibu Mkuu/ Hazina, Idara ya fedha za nje na Tume ya Mipango;
- Kubuni njia bora za kuandaa mijadala ya kibajeti inayohusiana na Mapato na matumizi kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
- Kubuni makadirio na makisio ya Mapato na matumizi ya Serikali kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
- Kusimamia muongozo wa utayarishaji wabajeti;
- Kuwasilisha nyaraka za bajeti kwa Makatibu Wakuu, Baraza la Mapinduzi (BLM) na Baraza la Wawakilishi (BLW);
- Kubuni mipango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni nyengine;
- Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.