MUUNDO UNAOPENDEKEZWA WA OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO
Muundo wa sasa wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango unaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango. Katika ngazi ya kiutendaji Wizara inaongozwa na Katibu Mkuu akisaidiwa na manaibu makatibu wakuu wawili (2), Idara nane (8), Ofisi Kuu Pemba na Vitengo sita (6). Aidha, Wizara ina jumla ya Taasisi nane (8) zinazojitegemea ambazo zipo chini ya Wizara hii, mchanganuo wa Idara, Ofisi Kuu Pemba, Vitengo na Taasisi Zinazojitegemea ni kama ifuatavyo: –
- Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
- Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.
- Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali.
- Idara ya Bajeti.
- Ofisi ya Msajili wa Hazina.
- Idara ya Fedha za Nje.
- Idara ya Sera za Kodi na Fedha
- Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
- Ofisi Kuu – Pemba.