Divisheni hii itakuwa itahusika na Usimamizi wa Mfuko Mkuu wa Serikali pamoja na uingizaji wa fedha kwa MaOfisi.
Majukumu ya Divisheni ya Usimamizi wa Fedha:
- Kusimamia na kutunza Mfuko Mkuu wa Serikali kulingana na Katiba na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma Na. 12, 2016.
- Kusimamia “Exchequer Release” na kutoa Fedha kwa, Idara na Taasisi za Serikali zinazopaswa kuingiziwa fedha kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinzohusika.
- Kuongoza utekelezaji wa taratibu za lazima za Kihasibu na miongozo yake.
- Kuandaa na kuwasilisha Jumuisho la Hesabu za Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
- Kufanya usuluhishi wa Hesabu za mapato na ulinganisho wa mapato hayo kwa Mamlaka (Taasisi) za ukusanyaji wa mapoto ya Kodi.
- Kushirikiana na Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kwa kuanzisha na kusimamia malimbikizo ya mapato yasiyo ya kodi.
- Kukadiria mahitaji ya Fedha za Serikali na kuhakikisha kuwa Fedha za kutosha zinapatikana kukidhi matumizi ya lazima ya Serikali kwa muda uliowekwa.
- Kuandaa uwasilishaji wa matarajio ya mapato na matumizi kwa Kamati ya Ukomo ya Serikali (Government Ceiling Committee).
- Kuandaa usuluhishi wa Kibenki kwa Hesabu zote za Hazina ya Serikali (Forex and Local Accounts).
- Kutayarisha taarifa zinazoonesha vifungu tofauti vya budget, Fedha iliyotengwa, hesabu na usimamizi wa kihasibu wa kila siku.
- Kudhibiti matumizi kwa kulinganisha na mapato na kuhakikisha uwepo wa ukwasi (Liquidity Position).
- Kuanzisha na kuweka daftari linaloonesha faida/hasara za Amana za Serikali.