Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Juma Malik Akil amewasitiza wastaafu watarajiwa kutumia vizuri mafao ya kustaafu katika uwekezaji sahihi ili kuhimili maisha kipindi cha uzeeni
Ambapo anazitaja kuwa ni jitihada za serikali katika kuwajali wastaafu na kuimarisha mfuko huo ili uendelee kuleta tija katika jamii
Tukio hili linaanza uzinduzi wa kitabu cha safari ya ustaafu ambapo ni dira ya kuwaongoza na kutafakari katika maisha yao baada ya kustaafu
Mara baada ya tukio hilo Dkt Akil anazungumza na wastaafu watarajiwa katika mafunzo ya maandalizi ya kustaafu kwa wastaafu watarajiwa watakaolipwa na mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar katika ukumbi wa zssf Michenzani Mall anasema wastaafu wawe watulivu wajiandae na maisha mapya baada ya kustaafu kwao
Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg. Nassor Shaaban Ameir anasema mafunzo hayo yataleta chachu ya kuwaondolea hofu wastaafu juu ya matumizi sahihi ya mafao hayo ili kuendelea kujiinua kiuchumi
Nao Wastaafu watarajiwa wamesema watakuwa makini na ushauri juu ya matumizi ya fedha zao za kustaafu