Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Bakari Hamad Bakari amewataka watendaji wa wizara hiyo kumpa mashirikiano ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi za Wizara ya Fedha na kuonana na wafanyakazi katika Idara na Vitengo tofauti.
Amesema ili kuweza kufanya kazi zake vizuri ni lazima kuwe na mashirikino mazuri na wafanyakazi ili kuweza kutatua changamoto zao.
Amewataka wafanyakazi hao kufanyakazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya nchi kuliko maslahi yao binafsi.
Hata hivyo amewataka wafanyakazi kupendana, kushirikiana na kuwa wabunifu katika kutekeleza kazi zao.
Nao wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wameahidi kumpa mashirikiano Naibu Waziri katika kutekeleza kazi zake.