Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Rais Fedha na Mipango

Uongozi na Usimamizi

WAZIRI:

Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Kifungu 42 (2) akiwa na jukumu Kusimamia na kuendeleza utekelezaji wa sera na mipango inayohusiana na sekta husika.

NAIBU WAZIRI:

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Kifungu 42 (2) akiwa na jukumu Kumsaidia Mhe. Waziri na kuendeleza utekelezaji wa sera na mipango inayohusiana na sekta husika.

KATIBU MKUU:

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu Nam.50 (2) na (3) akiwa ndie anaesimamia masuala ya jumla ya Fedha za Serikali pamoja na masuala ya kitaifa ya utafutaji misaada na mikopo kwa wahisani.

NAIBU KATIBU MKUU:

Naibu Katibu Mkuu atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa kazi za kila siku za Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, vile vile anasimamia Idara tisa (9) zenye Divisheni Thelathini na moja (31) na Vitengo tisa (9).

Scroll to Top