Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

wizara ya Fedha na Mipango

Habari & Matukio

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akil, amewataka maafisa manunuzi wa umma nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uzalendo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi na kuleta tija kwa taifa.

Dk. Malik aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Pili wa mwaka wa maafisa Ununuzi wa Umma Zanzibar katika ukumbi wa Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid (ZEC) Maisara

Alisema maafisa manunuzi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa shughuli za serikali kutokana na nafasi yao katika kusimamia matumizi ya rasilimali za umma.

Aidha alisema kada hiyo inapaswa kutambua wajibu wake wa msingi wa kusimamia sheria za manunuzi na kuhakikisha kila hatua ya mchakato wa ununuzi inafanyika kwa uwazi, uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Alisisitiza kuwa maafisa hao wanapaswa kutanguliza uzalendo na maslahi ya nchi badala ya maslahi binafsi, huku wakitekeleza majukumu waliyopewa kwa mujibu wa sheria na mikataba ya ajira.

Alisema serikali imekuwa ikipokea malalamiko kuhusu mikataba ambayo haitekelezwi ipasavyo au kushindwa kuilinda maslahi ya taifa hivyo aliwasisitiza  umuhimu wa kuandaa mikataba yenye tija na inayotekelezeka.

Dk. Akil alisema sekta ya manunuzi ni mhimili mkubwa wa utekelezaji wa shughuli za serikali kwani takribani asilimia 80 ya shughuli za serikali zinategemea huduma za wataalamu wa manunuzi.

Akizungumzia mageuzi ya mifumo, alisema serikali imeamua kuondokana na mifumo ya kienyeji kwa kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa e-Procurement System (ePROS) ili kuongeza uwazi, ufanisi na uwajibikaji katika manunuzi ya umma.

Aliahidi kuwa serikali inaendelea kuithamini kada ya manunuzi kwa kuimarisha mfumo wa kisheria na mamlaka zinazosimamia sekta hiyo, huku mipango ikiendelea ya kuanzisha chombo cha kitaaluma kitakachosajili maafisa wote wa manunuzi nchini.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza hadhi ya taaluma hiyo, kuimarisha uwajibikaji wa wataalamu na kuhakikisha maslahi yao yanazingatiwa sambamba na wajibu mkubwa walio nao katika kulinda rasilimali za taifa.

Alisema ni imani yake mkutano huo utazaa matunda kwa kada hiyo ili kuona

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dk.Hamad Omar Fakih, alisema dhamira kubwa ya serikali ni kuhakikisha manunuzi ya umma yanafanyika kwa uwazi na weledi kwani taasisi hiyo ni muhimu kwa serikali.

Aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa ili kuhakikisha maendeleo ya nchi yaliyokusudiwa yanafikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Mohammed Fakih Mzee, alisema maofisa hao wana nafasi ya kipekee kuhakikisha fedha ya umma inatumika na inaleta matokeo yaliyousudiwa.

Mapema Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa sera za Ununuzi wa Umma Zanzibar, Omar Said Omar, alisema mkutano huo umelenga kuimarisha uwazi wa ununuzi wa umma kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema ununuzi wa umma ni nyenzo muhimu na kichocheo cha kimkakati kwa maendeleo ya Zanzibar na kukua kwa uchumi.

Alibainusha kuwa lengo kuu ni kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati thabit katika utekelezaji  wa majukumu ya kila siku.

Alisema malengo mengine ni kuimarisha mifumo ya kielektoriniki na kushirikisha sekta binafsi.

Katika mkutano huo mada mbalimbali ziliwasilishwa ni pamoja na madhara ya rushwa kwa watumishi wa umma, changamoto ya mfumo wa kielktoriki wa katika ununuzi wa umma,

Scroll to Top