Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Bakari Hamad Bakari amewataka Wakandarasi wanaosimamia miradi mbalimbali ya Serikali kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara ya kutembelea Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF na kufanya kikao Ka kamati ya PAC ya Baraza la Wakilishi
Amesema mkandarasi ambaye anakwenda kinyume na sheria zilizowekwa na Serikali achukuliwe hatua bila kuonewa huruma huku akiutaka mfuko huo kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali.
Mwenyekiti wa kamati ya PAC Kombo Mwinyi Shehe ameutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF kuangalia Sheria na Miongozo ya utekelezaji wa Miradi inayosimamiwa na Serikali.
Amesema ili ufanisi uweze kupatikana ni lazima kuwe na utendaji kazi kwa bidii hasa ukizingatia kuwa taasisi hiyo ni kigezo cha taasisi nyengine.
Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF Ndg. Nassor Shaaban Ameir, amesema kua mfuko huo utaendelea kusimamia na kutekeleza miradi yake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha kunakuwepo na uwazi, uwajibikaji na ufanisi, pamoja na kuzuia vitendo vya ukiukwaji wa taratibu katika utekelezaji wa miradi hiyo.