ZIAAT Yatakiwa Kudhibiti Uadilifu wa Taaluma ya Uhasibu
Waziri Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akil ameilekeza Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wawashauri elekezi Zanzibar (ZIAAT)kusimamia Kwa karibu maadili na uwajibikaji WA Wahasibu ili kuondoa taswira hasi iliyoibuka Katika jamii kuhusu uaminifu wa Wahasibu Katika matumizi ya Fedha za Taasisi za Umma na Binafsi.
Dkt Juma aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kutemblea ofisi zilizo chini ya Wizara yake.
Amesema kumekuwepo na mitazamo mbalimbali mingoni mwa wananchi kuhusu taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi WA Fedha za Umma Hali inayosababiswa na baadhi ya Wahasibu wasikuwa wadilifu walikosa uzalendo na misingi ya maadili na kufanya Kazi kinyume na maadili ya taaluma yao.
Amesisitiza kuwa bodi hiyo inawajibikubwa wakusimamia ipasavyo uwadilifu na uwajibikaji WA taaluma hiyo ili kurejesha Imani ndani ya jamii akileza kuwa kazinya Uhasibu na Ukaguzi inahitaji kufwa Kwa kuzingtoa misingi ya Sera Sheria na taratibu zilizopo.










