Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

wizara ya Fedha na Mipango

Latest Events

Latest Events

ZIAAT Yatakiwa Kudhibiti Uadilifu wa Taaluma ya Uhasibu

ZIAAT Yatakiwa Kudhibiti Uadilifu wa Taaluma ya Uhasibu Waziri Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akil ameilekeza Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wawashauri elekezi Zanzibar (ZIAAT)kusimamia Kwa karibu maadili na uwajibikaji WA Wahasibu ili kuondoa taswira hasi iliyoibuka Katika jamii kuhusu uaminifu wa Wahasibu Katika matumizi ya Fedha za Taasisi za Umma na Binafsi. Dkt Juma aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kutemblea ofisi zilizo chini ya Wizara yake.Amesema kumekuwepo na mitazamo mbalimbali mingoni mwa wananchi kuhusu taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi WA Fedha za Umma Hali inayosababiswa na baadhi ya Wahasibu wasikuwa wadilifu walikosa uzalendo na misingi ya maadili na kufanya Kazi kinyume na maadili ya taaluma yao. Amesisitiza kuwa bodi hiyo inawajibikubwa wakusimamia ipasavyo uwadilifu na uwajibikaji WA taaluma hiyo ili kurejesha Imani ndani ya jamii akileza kuwa kazinya Uhasibu na Ukaguzi inahitaji kufwa Kwa kuzingtoa misingi ya Sera Sheria na taratibu zilizopo.

Latest Events

Serikali Yaitaka ZHSF Kuimarisha Uendelevu wa Kifedha

Serikali Yaitaka ZHSF Kuimarisha Uendelevu wa Kifedha WIZARA ya Fedha na Mipango Zanzibar, imeutaka Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) kuhakikisha unaendelea kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya huku ukidumisha uendelevu wa kifedha wa mfuko huo. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Wizara hiyo Dk.Juma Malik Akil wakati alipokutana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na watendaji wa mfuko huo, katika ziara yake ya kujitambulisha katika ofisi za mfuko huo Michenzani Moll. Alisema ni muhimu kwa mfuko kujipanga kikamilifu ili kuendelea kuwa endelevu (sustainable) kwani mifuko inayotoa huduma za kijamii mara nyingi hukumbwa na changamoto ya kupoteza uendelevu kutokana na ugumu wa kupima faida za huduma hizo. Aidha alisema uendelevu wa mfuko ni nguzo muhimu katika kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kutolewa kwa wananchi bila kuyumba. “Ni muhimu kujipanga vizuri ili mfuko uwe endelevu, kwani hilo litahakikisha huduma zinaendelea kutolewa kwa uhakika na kwa muda mrefu,” alisema. Dk.Juma alibainisha kuwa bado hana uhakika kama mfuko unaweza kuingia kwenye uwekezaji mkubwa kutokana na hatari (risk factors) zilizopo, hivyo alisisitiza fedha zinazopatikana zielekezwe kwenye miradi yenye tija na usalama zaidi. Hata hivyo, alisema serikali imefanya maboresho ya mfumo wa ukusanyaji wa fedha za wanachama, pamoja na kuandaa utaratibu maalum wa kushirikisha wadau mbalimbali ili kuongeza mapato ya mfuko, ambapo kwa awamu ya mwanzo umeanza kwa kuhusisha bima ya wasafiri. Aliahidi kwamba serikali itaendelea kutafuta watu ambao wataweza kusaidia mfuko ili kuongeza uwezo. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Hamad Omar, aliutaka mfuko huo kuhakikisha unasimamia kikamilifu sheria na kanuni zake, hususan kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika matumizi ya huduma za mfuko. Alisema yapo malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utoaji wa huduma pamoja na kutokuelewa mipaka ya huduma zinazotolewa na mfuko huo hivyo aliusisitiza mfuko kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma ili wananchi wawe na uelewa sahihi wa mfuko na haki zao. Aliwataka watendaji wa mfuko kutanguliza misingi ya uadilifu, uzalendo na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili lengo la kuanzishwa mfuko huo liweze kufikiwa Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar, Mbarouk Omar Mohammed, aliipongeza serikali kwa kuipa kipaumbele sekta ya afya kwani kuanzishwa kwa mfuko huo kumesaidia kuwapa wananchi uwezo wa kupata huduma za matibabu kwa urahisi zaidi. Alifahamisha kuwa hadi sasa mfuko umefanikiwa kusajili takribani asilimia 50 ya walengwa, huku asilimia nyingine ikiwa bado haijafikiwa, hususan kundi la wastaafu ambao wengi wao bado wako nje ya mfumo wa kupata mafao ya afya. Alisema bodi inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kundi hilo halibaki nyuma na kuiomba serikali kupitia wizara husika kulifanyia kazi suala hilo ili wastaafu nao waweze kunufaika na huduma za afya kupitia mfuko huo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa ZHSF, Khalifa Muumin Hilal, alisema mfuko huo unaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali wakati wa kuanzishwa kwake. Alieleza kuwa ZHSF imeanzishwa kwa mujibu wa sheria Namba 1 ya mwaka 2023, ikiwa na lengo la kuwa mfuko imara wa kuwawezesha wananchi wote kupata huduma za afya kwa uhakika. Aliongeza kuwa mpango wa mfuko ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi kwa kufungua ofisi 11 katika maeneo mbalimbali ikiwemo Tumbatu, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na ukusanyaji wa michango ya wanachama. Alifahamisha kuwa katika kipindi cha miaka miwili na nusu, mfuko ulilenga kusajili zaidi ya wanachama milioni moja (1,000,000), ambapo hadi Desemba mwaka jana, jumla ya wanachama 999,111 walikuwa tayari wameshasajiliwa. Kwa upande wa michango, alisema mfuko ulilenga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 1.4, lakini hadi sasa umefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 111. Hata hivyo, alibainisha kuwa mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo maslahi ya watendaji, matumizi mabaya ya kadi za wanachama, michango ya wastaafu, upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, pamoja na changamoto ya ofisi kwani kwa sasa mfuko unatumia jengo la kukodi. Alisema licha ya changamoto hizo, mfuko unaendelea kuimarisha mifumo yake ya kazi, kusajili vituo vya kutolea huduma na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya. Aliongeza kuwa hadi sasa jumla ya vituo vya afya 135 vimeshasajiliwa kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar na hata kwa Tanzania bara.

Latest Events

BOT Yasihiwa Kuimarisha Uchumi wa Kidijitali Zanzibar

BOT Yasihiwa Kuimarisha Uchumi wa Kidijitali SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema nchi inategemea kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato ya ndani hususan yatokanayo na kodi, ambayo hutumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wananchi. WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akil, aliyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Benki Kuu ya Tanzania Ofisi ya Zanzibar  mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea makao makuu ndogo Kinazini. Alisema mapato hayo ni mhimili muhimu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Dk. Juma alisema tafiti zilizofanywa na wataalamu kutoka Tume ya Mipango zimebaini kuwa Zanzibar inapoteza zaidi ya asilimia 83 ya mapato ambayo ingeweza kuyakusanya endapo kungekuwa na mifumo imara na ya kisasa ya ukusanyaji wa mapato. Alibainisha kuwa upungufu huo unatokana na kutokuwepo kwa mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato, hali inayosababisha serikali kukusanya takribani asilimia 17 tu ya uwezo wake halisi. Aidha alisema endapo mifumo ya kidijitali itatumika kikamilifu, kuna uwezekano mkubwa wa kufikia asilimia 100 ya makusanyo, hivyo kuziba pengo la upotevu wa mapato unaofikia asilimia 83 ambayo kwa sasa nchi inashindwa kuyakusanya na nchi inapoteza mapato yake. Akizungumza kuhusu umuhimu wa uchumi wa kidijitali, alisema ni lazima sekta ya fedha ihakikishe kila senti inayopaswa kukusanywa inakusanywa ipasavyo na kuelekezwa katika malengo yaliyokusudiwa, yakiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida ya serikali ili kuleta tija kwa wananchi wanaoitegemea serikali yao. Alibainisha kuwa matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali yataiwezesha nchi kujenga miradi mikubwa ya maendeleo bila kutegemea kwa kiasi kikubwa mikopo. “Nchi inaweza kujenga miradi yake mikubwa bila ya kukopa fedha nyingi hivyo  BOT  endeleeni kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna gani ya kutumia mifumo ya kisasa ya kifedha  ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali,” alisema Dk. Juma alisisitiza kuwa ni lazima nchi iendelee kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hususan ile ya kimkakati, akibainisha kuwa mapato ya ndani yakikusanywa ipasavyo yatakuwa chachu ya maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi kwa ujumla. Dk.Juma aliitaka BOT kuendelea kushirikiana kwa karibu na sekta mbalimbali za uchumi pamoja na taasisi za utafiti ili kufanya tafiti zenye tija zitakazosaidia kubaini fursa, changamoto na mikakati bora ya kukuza uchumi wa nchi. Alisema tafiti hizo ni nguzo muhimu katika kutoa mwelekeo sahihi wa sera za fedha na maendeleo kwa ujumla. Alisisitiza kuwa tafiti zinazozingatia hali halisi ya uchumi zitasaidia pia kuimarisha uthabiti wa kifedha na kudhibiti changamoto za mabadiliko ya soko la ndani na kimataifa. Aliongeza kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Benki Kuu katika kuimarisha tafiti na ukusanyaji wa takwimu sahihi ili kuweka mazingira wezeshi ya maendeleo ya kiuchumi kwani kufanya hivyo  nchi itaendelea kujenga uchumi imara. Alisema serikali imeunda Wizara ya  Mawasiliano Teknologia na Ubunifu ambayo imepewa jukumu mama la  kuhakikisha uchumi wa kidijitali unatumika ipasavyo. Aliipongeza BOT kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani mchango wao ni mkubwa kwa serikali hivyo uzalendo , uaminifu na uadilifu ndio msingi imara wa kuendeleza kukuza uchumi wa nchi. Akitoa taarifa ya utendaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mkurugenzi wa benki hiyo Ofisi ya Zanzibar Ibrahim Joseph Malogoi alisema benki kuu kimsingi jukumu lake ni kutekeleza kazi za msingi za nenki kuu ya Tanzania. Hata hivyo alisema Benki Kuu inaendelea kutekeleza jukumu lake la msingi kama mhifadhi na mlipaji mkuu wa SMZ na taasisi nyengine za SMT zinazofanya shughuli zake Zanzibar. “Katika kutimiza wajibu huu benki kuu imeendelea kuhakikisha usimamizi thabiti wa akaunti za serikali, uratibu wa miamala yote ya kifedha na utoaji wa huduma za kibenki kwa wakati na ufanisi,” alisema Hata hivyo, alisema hadi Disemba 2025 idadi ya benki za biasjara zinazofanya kazi Zanzibar ni 15 zenye mtandao wa matawi 43. Mkurugenzi Ibrahim alibainisha kuwa makao makuu ndogo ya BOT inaendelea kuhifadhi fedha za SMZ zinazotokana na kodi na zisizotokana na kodi na kuipatia serikali hali halisi ya kifedha kila siku ili iweze kufahya maamuzi sahihi na kuhifadhi, kutoa na kusambaza fedha kwa benki za biashara zilizopo Unguja na kusimamia shughuli za uendeshaji wa kituo cha usambazaji wa noti na sarafu kilichopo Pemba ili kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha katika mzunguko kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Majukumu mengine alisema ni kuhaulisha fedha na kutoa vitabu vya hundi kwa wizara na idaea mbalimbali za SMZ , kuchambua fedha ili kuzirudisja kwenye mzunguko wa fedha zilizo safi na kuziondoa kwenye mzunguko zile zilizochakaa na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzitambua alama za usalama za noti zao, utunzaji bora wa noti na sarafu na kuhimiza matumizi ya mifumo mengine ya malipo. Sambamba na hayo benki pia inafatilia mwenendo wa uchumi wa Zanzibar kwa kufanya uchambuzi ikiwemo uzalishaji, mwenendo wa mapato na matumizi ya serikali, maendeleo ya sekta ya nje, mwenendo wa deni la serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na maendeleo ya sekta ya fedha. Alifahamisha kuwa benki pia hufanya tafiti mbalimbali ikiwemo utafiti wa hali ya uwekezaji Zanzibar, itafiti wa sekta ya utalii, utafiti wa upatikanaji wa chakula na tafiti nyengine. Alisema katika mwaka huu wa fedha shughuli za miradi mbslimbsli ilipangwa kutekelezwa ambapo hadi kufikia Disemba mwaka 2025 benki kuu Zanzibar imeendelea kutimiza jukumu lakw la kusambaza fedha (noti na sarafu) ili kutosheleza mahitaji ya uchumi bila kusababisha mabadiliko ya kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma. Alisema katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2025 benki kuu ilisambaza jumla ya shilingi bilioni 465.6 kati ya fedha hizo bilioni 394.3 zilisambazwa kupitia ofisi ya Unguja na shilingi bilioni 71.3 kupitia kituo cha Pemba. Alisema pamoja na mafanikio hayo zipo baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ambazo ni pamoja  wananchi kutokuwa na uelewa mzuri kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania, kutokuwa na uelewa wa fersa za uwekezaji katika masomo ya kifedha, kutokuwa na uelewa wa kutosha wa kuzitambua noti halali na namna bora ya utunzaji wa fedha. Alisema ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya BOT una mchango mkubwa katika kuimarisha sekta ya fedha na kuleta utulivu wa kiuchumi.

Latest Events

Serikali Yaendelea na Mageuzi ya Bajeti na Usimamizi wa Fedha

Serikali Yaendelea na Mageuzi ya Bajeti na Usimamizi wa Fedha WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Juma Malik Akil, ameiomba kamati ya Bajeti na Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hisabu za Serikali (PAC) kuwa karibu na wizara ya fedha katika kuvilinda na kuvitetea vipaumbele ambavyo vitapendekezwa na serikali na baraza liweze kuvibariki. Dk.Juma aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa kamati hizo katika ukumbi wa Dk.Shein ZURA Maisara yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa serikali. Alisema serikali imepita katika mageuzi makubwa katika miaka mitano na haijasita kwani inahamu kufanya mageuzi makubwa zaidi hasa kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Aidha alisema katika kufanya hivyo wanaweza kuwa na mabadiliko katika utekengezaji wa bajeti zake kwani mwaka jana waliweza kufanya bajeti takriban trillion 6.9 ikiwa ni tofauti na bajeti za miaka mitano iliyopita. Alisema ndani ya bajeti hiyo pia waliweka vipaumbele hasa ambapo sehemu kubwa ya vipaumbele hivyo ni utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo mwaka jana wametekeleza kwa asilimia 63 ya bajeti nzima ukilinganisha na asilimia 37 ya kazi za kawaida za kila siku. ” Mnaweza kuona jinsi miradi ya maendeleo inavyoonekana wazi kwa kutumia mfumo huu wa kutoa kipaumbele katika bajeti zetu za serikali za miradi ya maendeleo,” alisema Alisema mwaka huu pia serikali ina vipaumbele vyake na tayari wameshaanza michakato wa kuvitengeneza kwa kipindi cha bajeti ya 2026/2027 na miaka mitano ijayo ambayo sehemu kubwa ni kutekeleza ilani ya CCM ya 2015/2030. Alisema pia serikali ina mkakati maalum katika kukusanya mapato kwani ndio roho ya serikali na bajeti ni mapato na matumizi na mara nyingi wamekuwa wakilenga zaidi kwenye matumizi. Waziri Malik alibainisha kuwa wanatamani kupitia kamati kuibua mbinu mpya za mapato kwani serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi kutokana na njia zilizoeleka. “Mtusaidie tufanye nini ili kuepuka upotevu huu wa mapato na kushindwa kukusanya kwa sababu mbalimbali ambazo nyengine inawezekana kama tutaweza kuzisimamia vizuri zaidi,” alisema. Alisema serikali hivi sasa inafanya mageuzi kutoka katika mfumo wa fedha taslim (Cash Base) na kutumia mfumo wa kielektroniki lengo ni kuimarisha utendaji baada ya kuona kasoro ambazo zilijitokeza katika mfumo uliopita hasa katika utambuzi wa mali za serikali na ahadi za kifedha zinazowekwa hazipati nafasi kuonekana wazi wazi wakati walipokuwa wakitumia. Alifahamisha kuwa lengo la kuhama huko na kwenda kwenye ‘Acruare Base Aproch’ ni kuhakikisha hayo yote yanapatikana na kwenda sambamba na taratibu za kidunia. Alisema ni matumaini yake kwamba wakipatiwa mafunzo wataweza kuyachukua na kuweza kuwasimamia vizuri zaidi katika utekelezaji wake. “Utekelezaji wa shughuli zetu za kila siku wizara inategemea sana msaada wa kamati zetu hizi mbili kwani zinagusa mnasaba wa utekelezaji wa majukumu yetu,” alisema. Hata hivyo, alisema siku za nyuma ipo mifano ambayo wanatafutiana katika mambo fulani kutokana na kukosa uelewa lakini anaamini watazungumza lugha moja hasa wakati wa kutengeneza bajeti, kutekeleza bajeti na hata kutathimini bajeti watakuwa pamoja na wizara kusaidia kujenga hoja ili watakapowasilisha bajeti zao wawe na wenzao ambao wanawasaidia ndani ya baraza. Dk. Juma akiizungumzia kamati ya PAC alisema wizara inapata changamoto wakati wanapopata ripoti za CAG hivyo ni matumiani yake kamati hiyo itaweza kuwasaidia mapema ili kusiwe na kasoro ambazo zinajitokeza. Alisema kamati hizo zina umuhimu mkubwa kwani zingusa moja kwa moja utendaji wa ofisi yao hivyo alizipongeza kamati hizo kwa kukubali kupokea mafunzo na kushiriki kikamilifu. Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali, Hamad Saleh Hamad, alisema mafunzo hayo yamelenga kutoa uelewa kwa kamati hizo juu ya sheria ya fedha ya usimamizi wa fedha za umma ya mwaka 2016. Alisema sheria hiyo ina mambo mengi lakini wameona wajikite katika maeneo matatu ambayo ni muhimu hasa usimamizi wa fedha za umma,usimamizi wa matumizi na matumizi ya viwango kwa taasisi za umma. Haya ni mambo ya msingi na yanahitaji upekee kwa wajumbe wa kamati hizi kuweza kuelewa lakini pia usimamizi wa fedha kwani ndio msingi mkuu wa matumizi ya serikali lakini pia kufuata viwango vya kimataifa kwani hilo ni takwa la kisheria. Katika mafunzo hayo mada mbalimbali ikiwemo usimamizi wa matumizi katika sekta za umma na usimamizi wa fedha za umma kutoka kwenye mfumo wa fedha taslim na kutumia mfumo wa kielektoniki.

Scroll to Top