Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Rais Fedha na Mipango

Latest News

Latest News

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum ameendesha kikao cha Jukwaa la Uchumi na Bajeti kwa upande wa Serikali kuu kwa mujibu wa sheria ya Fedha.

Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewataka wanasheria wote wa serikali na makatibu wakuu kuacha kusaini mkataba wowote wenye vipengele vya kodi na baadae kuomba kusamehewa kodi kwani hiyo sio kazi yao kwani msamaha wa kodi unatolewa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango na msamaha unautaratibu wake ambao upo kisheria . Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza hayo wakati akifungua Jukwaa la bajeti la mwaka 2024/2025 kwa serikali kuu liloshirikisha makatibu wakuu katika ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni. “Tufahamu kuwa kodi inayokusanya ndio sisi inayotulipa mishahara, huduma za afya, elimu na huduma nyengine za barabara, maji, pencheni zinatokana na hii kodi,” alisema. Hivyo, aliahidi kwamba Ofisi yake itaendelea kulisimamia jambo hilo ili kuona kunakuwa na nidhamu ya ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuangalia namna bora ya kuhakikisha kila mmoja anawajibika katika usimamizi wa sheria za kodi nchini. “Jambo hili tutaendelea kulisisitiza ili kufikia utekelezaji wa bajeti kwa zaidi ya asilimia 100 na jambo hili linawezekana ikiwa kila mmoja wetu atakuwa mlinzi wa kodi ambazo ni fedha za umma,” alisisitiza. Waziri Saada akizungumzia bajeti zinazotaarishwa kuzingatia masuala ya kijinsia alisema bado kuna muamko mdogo kuhusiana na utayarishaji wa bajeti unaozingatia jinsia hasa kunufaika kwa wanawake katika masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, afya na mambo mengine. Alisema pamoja na kujaribu kujenga uwezo kwa watendaji lakini jambo hilo bado halijafanikiwa hivyo Ofisi yake itahakikisha inaweka nguvu kubwa katika baadhi ya wizara tano ikiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Elimu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Wizara ya Uchumi wa Bluu ili kuona namna gani wataweza kutekeleza bajeti zinazozingatia jinsia. Mbali na hayo Waziri Saada alisema wizara italifanyia kazi eneo la manunuzi na eneo la mapato ili kuhakikisha manunuzi yote yanayofanywa serikalini yanazingatia sheria. “Mara hii tunakwenda kwenye bajeti ambayo ya uhalisia utaingiziwa fedha na kazi zako utaonesha unazotakiwa uzifanye kisingizio cha kuwa huna pesa hujafanya hicho kitakuwa kimeisha. Jukwa hilo limehudhuriwa na Viongozi wakuu wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango. Aidha, washiriki wa jukwaa hilo walimuomba Mwenyekiti kuzingatia mijadala yaoSambamba na hayo walisisitiza kuomba kuwa miradi ya kimkakati kusimamiwa na serikali kuu na sio Idara au Mashirika ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati. Jukwaa hilo lipo kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa fedha za umma ambapo mada mbalimbali za uchumi na matumizi ziliwasilishwa na kuzingatia matumizi na makusanyo ya bajeti kwa mwaka 2024/2025.

Latest News

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya azindua Bodi ya ZIAAT

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Novemba 3,2023 amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi (ZIAAT) katika Ukumbi wa taasisi hiyo uliopo katika jengo la iliyokuwa Ofisi ya Mfuko wa Barabara Maisara Mjini Zanzibar Mhe. Waziri amewataka wajumbe wa Bodi hiyo wawe wabunifu na wasimamie taasisi Kwa maslahi ya Umma pamoja na kufanya uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao. Dkt. Saada ameshauri kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa (ZIAAT) wapitie vizuri Sheria ya (ZIAAT) na wafanye maboresho ya kuingiza masuala ya miamala ya fedha katika Sheria za kiislam pamoja na mambo mengine Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Bw. Juma Amour Mohammed ameeleza kuwa Bodi itafanya kazi Kwa uweledi wa hali ya juu katika kuboresha tasnia ya uhasibu na Ukaguzi pamoja na kutoa elimu Kwa wajumbe wa Bodi ili wafahamu Sheria ya (ZIAAT) Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi CPA. Ame Burhan Shazil ameeleza kuwa taasisi hii imeanzishwa Kwa Sheria No 7 ya Mwaka 2022 malengo yake ni pamoja na kuongeza ubora wa huduma zitolewazo na (ZIAAT), kuwatambua na kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa kodi Katika hafla hiyo, pia alikuwepo Muwakilishi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi CPA Charles Masabu ambae ameitaka (ZIAAT) kufanya kazi zake kitaalamu zaidi na wakianza tu kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi ni vyema wakasajiliwa Kwa njjia ya kieletroniki na hili litarahisisha ukusanyaji wa Kodi Imetolewa naKitengo cha Habari na UhusianoOfisi ya Rais, Fedha n Mipango

Latest News

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya akutana na Uongozi wa ASA Microfinance Limited

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Oktoba 26, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kifedha (ASA Microfinance Limited) Bibi Karin A. M.Kersten) ambae ameambatana na wajumbe mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa ASA Kwa upande wa Tanzania Ndg Muhammad Shah Newaj Bibi Kersten ameeleza kuwa Uongozi wa ASA umefika Ofisini Kwa Mhe. Waziri Kwa lengo la kujitambulisha na kueleza kuwa Kwa upande wa Tanzania Ofisi za ASA Microfinance Limited zinapatikana Kinondoni, Jijini Dar es Salaam Aidha, Bibi Kersten ameendelea kueleza kuwa Kwa upande wa Zanzibar Ofisi za ASA zinapatikana Maungani, Wilaya ya Magharib ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharib Dkt Saada Mkuya ameushukuru Uongozi wa ASA Kwa kufungua tawi lake Kwa upande wa Zanzibar kwani itakuwa ni fursa Kwa wajasiriamali wa sekta mbalimbali hasa sekta ya Uchumi wa Buluu kwani ndio kipaumbele Cha kuwakomboa Wazanzibari wengi ambao wanajishhhulisha na kilimo Cha mwani na uvuvi wa kawaida. Imetolewa naKitengo cha Habari na UhusianoOfisi ya Rais, Fedha na Mipango

Scroll to Top