Divisheni ya mageuzi ya bajeti inashughulika na kusimamia masuala ya sheria katika usimamizi wa fedha za Umma.
Majukumu ya Divisheni ya Mageuzi ya Bajeti
- Kusimamia masuala ya Sheria katika usimamizi wa fedha za Umma;
- Kuratibu MTEF na mpango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni;
- Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na ya mwaka.
- Kusimamia uimarishaji wa bajeti ya Serikali;
- Kubuni mfumo bora wa bajeti unaozingatia program;
- Kusimamia mageuzi yoyote yanayoigusa bajeti ya Serikali.