Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

Majukumu ya Divisheni ya Uendeshaji

  • Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi;
  • Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi;
  • Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Ofisi ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano;
  • Kusimamia majengo na mali za Ofisi;
  • Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Ofisi;