Divisheni hii inashughulika na kuwapatia ushauri Mawizara, Taasisi, Mashirika na Wakala juu ya kazi za kifedha na uhasibu.

Majukumu ya Divisheni ya Uhasibu na Utawala

 • Kutoa ushauri kwa Taasisi za Serikali kuhusiana na Uongozi na kazi za kifedha na kihasibu.
 • Kusimamia na kufuatilia huduma za kifedha na kihasibu zikiwemo maadili ya kitaaluma kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma Na. 12 ya mwaka 2016 na Kanuni zake pamoja na miongozo ya Kitaifa na Kimataifa.
 • Kuhakikisha kuwepo kwa masharti bora ya usalama wa Fedha, dhamana, nyaraka za mapato, leseni na nyaraka nyenginezo.    
 • Kufanya uchunguzi toshelevu ukiwemo ukaguzi wa kushtukiza kwa Taasisi za Serikali ili kuhakikisha kwamba Kanuni, maelekezo na miongozo inayohusiana na utunzaji wa Fedha, vifaa na mali za Umma zinaendana na Sheria na zinadhibitiwa kutokana na upotevu.    
 • Kutoa usimamizi na msaada wa kitaalamu kwa Wahasibu wa Serikali na kufanya uhamisho wa Wahasibu na Maafisa Fedha ndani ya Taasisi za Umma.
 • Kuhakikisha na kupanga wafanyakazi wenye uwezo wa kihasibu na Fedha katika Taasisi za Umma na kuwaongezea ujuzi wa kitaalamu wa muda mfupi na mrefu.  
 • Kusimamia ufunguzi na uendeshaji wa Hesabu za Serikali na kufuatilia bakaa la hesabu hizo.
 • Kufuatilia na kuratibu Bodi ya Uchunguzi wa Fedha taslim na Stamp na kutoa mapendekezo.
 • Kushirikiana na Kamati za Uchunguzi wa Hesabu za Serikali na Kamati ya Fedha za Baraza la Wawakilishi zinazohusiana na maswala yaliyopo na yanayojitokeza katika Kamati.
 • Kuongoza, kuratibu na kutekeleza shughuli zote za mageuzi ya usimamizi wa Fedha za Umma katika Taasisi za Umma.
 • Kusajili, kutathmini na kusimamia kampuni binafsi za kihasibu na kodi.
 • Kutathmini ufuataji wa Sheria ya Fedha, Kanuni na viwango vya usimamizi wa kihasibu vya kimataifa na washauri wa kodi kwa huduma wanazotoa.