Majukumu ya Uratibu wa Misaada

  • kusimamia sera na miongozo yote ya misaada ya nje ya kutoka kwa washirika wa maendeleo.
  • kusimamia na kuratibu usimamizi wa madeni ya nje ikiwemo kuweka kumbukumbu za mikataba ya mikopo pamoja na kufanya uchambuzi wa awali na kutoa ushauri wa kitaalamu wa mkopo husika.
  • kuratibu na kusimamia miradi   yote inayotekelezwa na idara ya fedha za nje.
  • kusimamia utayarishaji wa mipango na uteke lezaji wake na idara na kuandaa bajeti ya idara
  • kusimamia utayarishaji wa bajeti ya serikali na kushirikisha mchango wa washirika wa maendeleo katika bajeti ya maendeleo
  • kukusanya na kupokea na kuzifanyia uchambuzi wa taarifa kutoka kwa washirika wa maendeleo na kuandaa ripoti kutokana taarifa hizo.
  • kuratibu mikutano robo mwaka kwa sekta mashirika pamoja na taasisi za serikali na zisizo za serikali kwa ajili kukusanya taarifa za fedha pamoja na utekelezaji kutoka kwa washirika wa maendeleo
  • kufanya ufuatiliaji wa mikakati ya misaada kutoka nchi husika kutoka washirika maendeleona husisha pamoja na mipango yetu na utekelezaji
  • kuratibu mikutano ya majadiliano ya mwaka na ile ya nusu mwaka ya washirika wa maendeleo
  • kushirikiana na tume ya mipango katika uratibu wa kuonainisha malengo ya endelevu pamojana kuoanisha utekelezaji wa muongozo mpya wa mashirikiano baina ya serikali na washirika wa maendeleo.