Divisheni hii inashughulika na kuendeleza na kusimamia Sera za Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili ambazo zinakwenda sambamba na Ukuaji wa Uchumi.

Majukumu ya Divisheni ya usimamizi wa Sera.

  1. Kutathmini, Kuchambuzi na Kukadiria Mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
  2. Kufanya Uchambuzi wa Mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
  3. Kufanya makadirio ya mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili; na
  4. Kusimamia na Kufatilia mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
  5. Kusimamizi na Kupendekeza Sera za Mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
  6. Kupendekeza Miongozo ya Fedha juu ya Usimamizi wa Mapato na Matumizi Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili; na
  7. Kupendekeza Wigo wa Kutozea Kodi kwa Makampuni ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili.