Divisheni ya utekelezaji na ufuatiliaji wa bajeti inashughulika na kusimamia upatikanaji wa taarifa sahihi za mapato na matumizi ya Serikali.

Majukumu ya Divisheni ya Utekelezaji na Ufuatiliaji wa Bajeti

  • Kusimamia taarifa za Mapato na matumizi halisi za Mawizara na Taasisi;
  • Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya robo mwaka, nusu mwaka na ya mwaka;
  • Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali;
  • Kubuni mpango kazi na mpango wa maombi ya fedha kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
  • Kusimamia uingizwaji wa fedha ndani ya mfumo mjumuwiko wa fedha (IFMS);
  • Kusimamia matumizi kwa kila robo mwaka na kuiwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
  • Kuratibu utekelezaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Ofisi ya Mhasibu Mkuu/ Hazina, Idara ya fedha za nje na Tume ya Mipango;
  • Kubuni mipango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni nyengine;
  • Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.