Divisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

Majukumu ya Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu

 • Kuhifadhi Majalada yaliyofungwa kwa Kumbukumbu za baadae.
  • Kutafuta Kumbukumbu/Nyaraka/Mafaili yanayohitajiwa na watumishi wa Ofisi
  •  Kupokea na kudhibiti na kutunza kumbukumbu za Ofisi
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika makundi kulingana na mada husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi;
  • Kuweka/kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika Masjala na vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu tuli za Ofisi
  • Kuweka na kutunza kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika Mafaili;
  • Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka kwa maafisa mbali mbali na Taasisi za Serikali;
  • Kuhifadhi Majalada yaliyofungwa kwa Kumbukumbu za baadae.