Idara hii inasimamiwa na Kamishna ambae huteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Idara hii ina jukumu la kuandaa, kufatilia, kutekeleza, kufanya mageuzi ya bajeti pamoja na kudhibiti na kufatilia taarifa za mishahara za Watumishi wa Serikali.

Majukumu ya Idara ya Bajeti;

  1. Kuratibu uwasilishwaji wa bajeti za Mawizara na kusimamia uingizwaji wa taarifa za bajeti kwenye mfumo wa kielectroniki;
  2. Kusimamia uchapishaji wa hutuba ya bajeti ya Serikali pamoja na makadirio ya Mapato na matumizi;
  3. Kuratibu mswada wa fedha na matumizi;
  4. Kuratibu utekelezaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Ofisi ya Mhasibu Mkuu/ Hazina, Idara ya fedha za nje na Tume ya Mipango;
  5. Kubuni njia bora za kuandaa mijadala ya kibajeti inayohusiana na Mapato na matumizi kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
  6. Kubuni makadirio na makisio ya Mapato na matumizi ya Serikali kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
  7. Kusimamia muongozo wa utayarishaji wabajeti;
  8. Kuwasilisha nyaraka za bajeti kwa Makatibu Wakuu, Baraza la Mapinduzi (BLM) na Baraza la Wawakilishi (BLW);
  9. Kusimamia taarifa za Mapato na matumizi halisi za Mawizara na Taasisi;
  10. Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya robo mwaka, nusu mwaka na ya mwaka;
  11. Kusimamia utekelezaji wa bajeti ya Serikali;
  12. Kubuni mpango kazi na mpango wa maombi ya fedha kwa Wizara na Taasisi za Serikali.
  13. Kusimamia uingizwaji wa fedha ndani ya mfumo mjumuwiko wa fedha (IFMS);
  14. Kusimamia masuala ya Sheria katika usimamizi wa fedha za Umma;
  15. Kuratibu MTEF na mpango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni;
  16. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na ya mwaka.
  17. Kusimamia uimarishaji wa bajeti ya Serikali;
  18. Kubuni mfumo bora wa bajeti unaozingatia program;
  19. Kubunia njia bora za usimamizi ripoti za mishahara (CPO) Kwa ajili ya matayarisho ya malipo;
  20. Kuratibu uchapishaji wa taarifa za mshahara kwa kila mfanyakazi;
  21. Kusimamia uandaaji MTEF na mpango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni; 
  22. kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka
  23. Kuratibu marekebisho yaliyoidhinishwa ya wafanyakazi ndani ya Database ya mishahara;
  24. Kubuni njia bora ya uwasilishaji wa taarifa za  mishahara kwa kila mwezi kwa Taasisi husika za Serikali;

Idara hii inaundwa na Divisheni Kuu nne (4) ambazo ni: –

  1. Divisheni ya Uandaaji Bajeti
  2. Divisheni ya Utekelezaji na Ufatiliaji Bajeti;
  3. Divisheni ya Mageuzi ya Bajeti
  4. Divisheni ya Uthibiti na Uhifadhi