Idara hii inasimamiwa na Kamishna ambae huteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Idara hii inahusika na Kupitia Maandiko mbalimbali ya Miradi ya Kimkakati ili kuweza kutafutia Ufadhili kutoka washirika wa Maendeleo.

Majukumu ya Idara ya Fedha za Nje

  • Kupitia Maandiko mbalimbali ya Miradi ya Kimkakati ili kuweza kutafutia Ufadhili kutoka washirika wa Maendeleo.
  • Kuratibu Mikutano ya Mashauriano na Wizara Mbalimbali Ili Kuweza Kuibua Mradi ya Kimkakati Kulingana Na Fursa Zilizopo Za Ufadhili.
  • Kushirikiano Na Tume Ya Mipango Kupambanua Vipaumbele Vya Nchi Ambavyo Vinaweza Kupata Ufadhili Wa Washirika Wa Maendeleo.
  • Kuandaa Mpango Kazi Wa Ufuatiliaji Na Thathmini Wa Miradi Ya Washirika Wa Maendeleo Kila Robo Mwaka
  • Kufanya Ufuatiliaji Wa Miradi Ya Maendeleo Kifedha Na Utekelezaji wake, Kwa Kuangalia Upatikani Wa Fedha Za Washirika Wa Maendeleo.
  • Kuyatarisha Ripoti Za ufutailiaji Wa Miradi Mwezi. Robo Mwaka, Nusu Mwaka Na Mwaka Kutoka Kwa Washirika Wa Maendeleo
  • Kufuatilia Utekelezajia Wa Mpango Kazi Wa Idara.
  • Kusimamia Sera Na Miongozo Yote Ya Misaada Ya Nje Ya Kutoka Kwa Washirika Wa Maendeleo.
  • Kusimamia Na Kuratibu Usimamizi Wa Madeni Ya Nje Ikiwemo Kuweka Kumbukumbu Za Mikataba Ya Mikopo Pamoja Na Kufanya Uchambuzi Wa Awali Na Kutoa Ushauri Wa Kitaalamu Wa Mkopo Husika.
  • Kuratibu Na Kusimamia Miradi   Yote Inayotekelezwa Na Idara Ya Fedha Za Nje.

Idara ya Fedha za Nje inaundwa na Divisheni Kuu tatu (3), kama ifuatavyo: –

  1. Divisheni ya Utafutaji Rasilimali
  2. Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmin
  3. Divisheni ya Uratibu wa Misaada