Idara hii inasimamiwa na Kamishna ambae huteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ikiwa na jukumu la kusimamia Sera, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia udhibiti, utunzaji, utumiaji na uondoaji wa Mali za Serikali

Majukumu ya Idara ya Mitaji ya Umma.

 • Kusimamia Sera, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia udhibiti, utunzaji, utumiaji na uondoaji wa Mali za Serikali;
 • Kukagua na kudhibiti Mali za Serikali;
 • Kubuni na kurekebisha mifumo ya uwekaji wa Kumbukumbu za Mali za   Serikali.
 • Kumshauri mlipaji mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu usimamizi wa Mali za Serikali.
 • Kushauri na kusimamia ufutaji na uondoshaji wa Mali za Serikali.
 • Kuhakiki na kuthamini Mali za Serikali.
 • Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mashirika ya Umma
 • Kuchambua taarifa za kifedha, kiutekelezaji, Mipango Mkakati na Bajeti za kila mwaka za Mashirika ya Umma;
 • Kufuatilia mwenendo mzima wa kibiashara ili kuhakikisha Mashirika ya Umma  yanalipa gawio Serikalini;
 • Kuandaa na kutoa miongozo mbalimbali itakayopelekea kuongeza ufanisi katika Mashirika ya Umma;
 • Kusimamia Mashirika ya Umma ili kuhakikisha yanapunguza matumizi yasio ya lazima;

Idara hii imeundwa na Divisheni kuu mbili (2) ambazo ni:-

 1. Divisheni ya Usimamizi wa Mali za Serikali.
 2. Divisheni ya Mitaji ya Umma.