Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa 2022-2023, Sekta hii imetengewa jumla ya
TZS 53.59 bilioni miongoni mwa shughuli zinazokwenda kutekelezwa ni pamoja
kuimarisha huduma za matrekta ili kuweza kutoa huduma kwa wakati kwa mabonde
yenye ukubwa wa ekari 9,000 kwa Unguja na ekari 8,400 kwa Pemba kwa lengo
la kuongeza uzalishaji. Sambamba na hilo kwa mwaka ujao Serikali imedhamiria
kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji katika mabonde yenye ukubwa wa hekta
370 na kuunga umeme wa njia kubwa bonde la Cheju B.Sekta ya Usafirishaji

50. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Usafirishaji ni sekta ambayo ni chachu katika
kukuza uchumi wetu hapa nchini. Sekta hii inajumuisha, usafiri wa baharini,
usafiri wa nchi kavu na usafiri wa Anga. Kwa upande wa usafiri wa baharini tayari
Serikali inaendelea na mikakati ya kuendelea na uwekaji wa miundombinu rafiki
ili kuruhusu Ujenzi wa Bandari jumuishi itakayojengwa Mangapwani. Aidha, SMZ
tayari imekamilisha ujenzi wa Gati ndogo katika Bandari ya Mkokotoni ambayo
ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa maadhimisho ya Sherehe za
miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.