Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe Dkt Saada Mkuya Salum leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Ndg. Nathan Balete

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe Dkt Saada Mkuya Salum leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Ndg. Nathan Balete mazungumzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango

Mhe Dkt. Saada akiwa na mgemi wake wamejadili kwa pamoja Miradi ya Maendeleo ambayo inafadhiliwa na benki ya Dunia ikiwemo miradi inayoendelea na Miradi ya vipao mbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo miradi ya kuimarisha Nishati mbadala( ZEST)

Mradi wa kuimarisha miundombinu ya maji Unguja na Pemba, Mradi wa Elimu ambao unatekelezwa kwa pamoja na Tanzania bara mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kusomea kwa vyuo vikuu kwa kujengwa miundombinu mbalimbali

Aidha Dkt. Saada ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuleta maendeleo ya haraka hapa nchini.

Mhe dkt. Saada amesema Mradi wa sekta ya Afya utasaidia kuboresha vituo vya afya nchini, na kujenga uwezo wa madaktari na madaktari bingwa sambamba na kutatua changamoto za mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.

Mkurugenzi Nathan atakuwa na ziara ya siku mbili hapa Zanzibar akikagua Miradi iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia

Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango

Tags: No tags

Comments are closed.