Idara hii inahusika na utoaji wa huduma za uendeshaji na utumishi, kusimamia maslahi ya rasilimali watu, pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Uendeshaji na Utumishi

 • Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali watu na Utawala kwa Ofisi;
 • Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Ofisi;
 • Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji;
 • Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Ofisi na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum;
 • Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (UKIMWI, jinsia, Mabadiliko ya tabianchi na mambo ya idadi ya watu);
 • Kuhifadhi na kutunza kumbukumbu zote za Ofisi;
 • Kusimamia rasilimali zote za Ofisi;
 • Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa mteja.
 • Kushughulikia na kukadiria upatikanaji wa mahitaji, vifaa na vitendea kazi na kuhakikisha vinatunzwa na kutumika ipasavyo;
 • Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa huduma kwa umma;
 • Kuandaa na kutunza kumbukumbu za watumishi;
 • Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya mafunzo;
 • Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi;
 • Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi; na
 • Kuratibu utekelezaji wa upimaji utendaji kazi.
Client

Delta

Release Date

Feb 2019

Role

App Design