Divisheni hii itahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani Ofisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi, upandishaji vyeo. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Majukumu ya Divisheni ya Utumishi
- Kutunza Kumbukumbu sahihi za Watumishi wote kulingana na mahali alipo
- Kukusanya Takwimu na kutunza Kumbukumbu zote zinazohusu Mipango ya Watumishi na watumishi wenyewe
- Kukadiria idadi ya Watumishi wanaohitaji Mafunzo
- Kuratibu na Kushughulikia ajira, uthibitishwaji kazini na upandishwaji Vyeo Maofisa wa ngazi mbali mbali
- Kufuatilia na kudhibiti Kumbukumbu za Maafisa wanaokaribia kustaafu Pamoja na kutafiti uwezekano wa upatikanaji wa nafasi za Mafunzo vyuoni
- Kuandaa makisio ya Mishahara ya Watumishi kwa kila mwaka
- Kupanga na kuendesha utafiti kuhusu mahitaji ya Watumishi na upatikanaji wa Watumishi ili kuweza kuainisha uwezo na mahitaji ya Ofisi
- Kufuatilia masuala ya uthibitishaji kwa watumishi, upandishaji vyeo, uhamisho, ubadilishaji kada, kustaafisha, likizo na mengineyo.
- Kuandaa ikama (norminal roll) itakayojumuisha makadirio ya mishahara ikiwemo mahitaji halisi ya watumishi pamoja na maslahi ya watumishi wa Baraza.
- Kushughulikia maslahi mbali mbali ya watumishi katika taasisi.
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa urithishaji madaraka (succession plans).
- Kushughulikia masuala yote ya kiutumishi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo, upimaji utendaji kazi.
- Kushughulikia malalamiko, migogoro na matatizo ya wafanyakazi.
- Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa Miundo ya Utumishi na taasisi.