VYEO, SIFA, MAMLAKA YA UTEUZI NA MASLAHI YA VIONGOZI KATIKA MUUNDO WA OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO.

Kuhusu Vyeo, Sifa, Mamlaka ya Uteuzi wa Viongozi wa Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango itakuwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Miongozo mbali mbali inayotumika katika Utumishi wa Umma.

Aidha, kuhusu Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Divisheni watateuliwa na Katibu Mkuu kufuatia mapendekezo ya Wakurugenzi wa Idara. Sifa ya kuteuliwa kwao ni kupendekezwa kwa mtumishi mwenye uzoefu wa kazi wa angalau Daraja la Afisa Mwandamizi katika kada inayohusiana na majukumu ya kitengo au divisheni husika.

Mishahara na Maslahi ya Viongozi wote wanaopendekezwa katika muundo yatakuwa kwa mujibu wa matoleo na miongozo kutoka Serikalini.