Idara hii inasimamiwa na Mkurugenzi ambae huteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Sera za Kodi na Fedha

 • Ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wake na pia kukadiria athari za mapato kutokana na mikakati ya hatua mbalimbali za kuimarisha mapato na kuhakikisha hali nzuri na imara ya kodi ndani ya uchumi.
 • Kufuatilia na kushauri Serikali juu ya usimamizi wa mapato yatokanayo na Kodi na mapato yasiyokuwa ya kodi kwa Taasisi zinakusanya mapato na kupendekeza hatua za kukabiliana na hatua za kukwepa kodi na ukwepaji wa kodi.
 • Kufanya uchambuzi wa mapato na kufanya makadirio ya mapato yatokanayo na kodi na yasiyokuwa ya kodi katika kuhakikisha utulivu wa sera za kodi na matumizi.
 • Kushauri Serikali juu ya Ugawanyaji wa Fedha pamoja na uhusiano kati ya Serikali kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
 • Kufanya Uchambuzi wa Mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
 • Kufanya makadirio ya mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili; na
 • Kusimamia na Kufatilia mapato Yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili;
 • Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa sekta ya benki katika maendeleo ya uchumi.
 • Kushauri, Serikali juu ya zana madhubuti za kuzuia matumizi mabaya ya mfumo wa kifedha, uhalifu wa kifedha pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.
 • Kushiriki na kushauri juu ya mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa juu ya maendeleo ya sekta ya benki
 • Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sekta ya Bima na Masoko ya Mitaji, katika maendeleo ya uchumi.
 • Kuchukua hatua sahihi katika kuboresha uimara wa kifedha na sekta isiyo ya benki.

 Idara hii inaundwa na Divisheni zifuatazo: -.

 1. Divisheni ya Sera ya Kodi
 2. Divisheni ya Usimamizi wa Sera za mapato.
 3. Divisheni ya Usimamizi wa Sera za Fedha