Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano ndani Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.  Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.

Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari

 • Kusimamia muundo na mpangilio ya Sheria na taratibu katika kuendeleza na kutumia mfumo wa mawasiliano ya habari;
 • Kufanya uchambuzi na kubuni mifumo ya kiteknolojia, habari na mawasiliano ya kusaidia Ofisi kuweza kutoa huduma na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu;
 • Kuandaa na kutekeleza mkakati wa kiteknolojia, habari na mawasiliano pamoja na kufanya tathmini;
 • Kufanya ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa Sera ya teknolojia, habari na mawasiliano;
 • Kuhakikisha mipango ya uanzishwaji na uendelezaji wa teknolojia ya mawasiliano ipo katika hali nzuri na yenye gharama nafuu;
 • Kutunza, kutoa ushauri na kuratibu ununuaji wa vifaa (hardware) vya kiteknolojia, habari na mawasiliano pamoja na programu (software);
 • Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi bora ya mfumo wa mawasiliano ya habari (hardware & software);
 • Kuanzisha, kuratibu na kuelekeza matumizi ya barua pepe;
 • Kuanzisha na kuwezesha matumizi ya mtandao kiambo ‘Local Area Network (LAN)’ na mtandao mpana ‘Wide Area Network (WAN)’;
 • Kuandaa na kutunza ‘web-portal’ na mtandao wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
 • Kutengeneza na kuhakikisha matumizi salama ya mfumo na vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano;
 • Kutayarisha njia ya utaratibu mzuri wa kuboresha utendaji na utoaji wa huduma na utekelezaji kazi za Ofisi kupitia mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano;
 • Kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya utumiaji wa mifumo na vifaa vya kiteknolojia, habari na mawasiliano;
 • Kuratibu maendeleo ya uhifadhi wa program katika kuhakikisha usalama wa taarifa;
 • Kufanya tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa habari na mawasiliano katika Ofisi;
 • Kutunza Kumbukumbu za mfumo wa matumizi ya Kompyuta; na
 • Kusimamia na kuendesha tovuti ya Serikali.