Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya utayarishaji na ufanyaji malipo mbali mbali ndani ya Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.

Majukumu ya Kitengo cha Uhasibu

  • Kuhakikisha usimamizi bora wa mapato yote na matumizi ya kazi za kawaida na maendeleo ya fedha za Ofisi pamoja na washirika wa maendeleo;
  • Kufuatilia upatikanaji wa fedha kutoka Vyombo vinavyohusika;
  • Kuhakikisha fedha zinatumika kwa mujibu wa MTEF na Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
  • Kuandaa na kufanya malipo mbalimbali;
  • Kuandaa taarifa zote za uhasibu na kuwasilisha kunakohusika kwa wakati;
  • Kuratibu na kusimamia ‘VOTE’ zilizo chini ya Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
  • Kutoa ushauri wa kiuhasibu kuhusiana na mambo yote ya fedha; na
  • Kusimamia rasilimali fedha, na shughuli zote za uhasibu kwa mujibu wa Sheria za Fedha pamoja na Sheria ya Ununuzi na Uondoshaji wa mali ya Umma pamoja na Kanuni zake.
  • Kuratibu na kusimamia vyanzo vya mapato.