Divisheni ya usimamizi wa mali za Serikali inashughulika na usimamizi wa sera, kanuni na miongozo inayosimamia udhibiti, utunzaji, na uondoaji wa mali za Serikali.
Majukumu ya Usimamizi wa Mali za Serikali
- Kusimamia Sera, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia udhibiti, utunzaji, utumiaji na uondoaji wa Mali za Serikali;
- Kukagua na kudhibiti Mali za Serikali;
- Kubuni na kurekebisha mifumo ya uwekaji wa Kumbukumbu za Mali za Serikali.
- Kumshauri mlipaji mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu usimamizi wa Mali za Serikali.
- Kushauri na kusimamia ufutaji na uondoshaji wa Mali za Serikali.
- Kuhakiki na kuthamini Mali za Serikali.
- Kutunza daftari la jumla la Kumbukumbu za Mali za Serikali.
- Kuandaa Mafunzo kwa Wizara na Taasisi juu ya usimamizi na utunzaji wa Mali za Serikali.
Kuhakiki taarifa za Mali za Serikali zilizopo katika Wizara na Taasisi zake kabla ya kuingizwa katika Daftari la la jumla la Mali za Serikali