Divisheni ya Mitaji ya Umma inashughulika na kusimamia, kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mashirika ya Umma

Majukumu ya Divisheni ya Mitaji ya Umma.

Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mashirika ya Umma

  • Kuchambua taarifa za kifedha, kiutekelezaji, Mipango Mkakati na Bajeti za kila mwaka za Mashirika ya Umma;
  • Kufuatilia mwenendo mzima wa kibiashara ili kuhakikisha Mashirika ya Umma  yanalipa gawio Serikalini;
  • Kuandaa na kutoa miongozo mbalimbali itakayopelekea kuongeza ufanisi katika Mashirika ya Umma;
  • Kusimamia Mashirika ya Umma ili kuhakikisha yanapunguza matumizi yasio ya lazima;
  • Kuishauri Serikali juu ya namna bora ya kuongeza mtaji katika Mashirika ya Umma;
  • Kusajili Mashirika ya Umma pamoja na kutunza daftari la usajili;
  • Kufuatilia utekelezaji wa miradi inayoanzishwa na Mashirika ya Umma;
  • Kusimamia Mitaji ya Umma pamoja na Hisa za Serikali katika Kampuni Binafsi;
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Mitaji ya Umma;
  • Kusimamia program ya Ujenzi wa Ofisi za Serikali.