Divisheni hii inahusika na shughuli za ukusanyaji wa taarifa na kutayarisha Mipango ya kisekta, kuandaa bajeti, kutayarisha taarifa ya utekelezaji. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

Majukumu ya Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo

  • Kukusanya taarifa na kutayarisha Mpango wa Kazi wa Mwaka pamoja na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Ofisi kwa kushirikiana na Tume ya Mipango ili kuhakikisha mipango hiyo inakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya Kitaifa ikiwemo MKUZA II na Dira ya 2050;
  • Kuratibu utayarishaji wa mpango mkakati na utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi;
  • Kukusanya Taarifa za Miradi, Programu na Mipango kazi ya Ofisi;
  • Kujenga uelewa na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Ofisi na kutayarisha Bajeti ya Ofisi;
  • Kukusanya taarifa za mapitio ya utekelezaji za kipindi cha muda wa Kati na Mwaka za Ofisi;
  • Kukusanya taarifa na Takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya Uchumi, ustawi na maendeleo ya jamii;
  • Kuratibu utekelezaji wa maamuzi ya Serikali juu ya masuala ya Mipango na Uongozi wa masuala ya kiuchumi ya Ofisi;
  • Kukusanya Taarifa na Takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi na maendeleo ya jamii;
  • Kuchambua na kutafsiri (interpret) Takwimu na Taarifa mbalimbali za kiuchumi.