Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo tarehe 2/05/2024 imetiliana saini na kampuni ya CRJE juu ya Mkataba wa Ujenzi Mradi wa Uimarishaji wa Miji Kwa Upande wa Unguja.
Kwa niaba ya Serikali Mkataba huo umewekwa saini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil ambapo jumla Bilioni 40,535,043,304.24 zinatarajiwa kutumika kwa ujenzi wa maeneo ya Sebleni – Kwa Wazee, Meya- Magomeni na Mtaro wa Mfumo C, kwa upande wa CRJE mkaba huo umesainiwa na XU Chang ambae ni Meneja wa kampuni.
Mradi huo utaipa hadhi na kuyakuza maeneo ya Mjini kwa i ) kujenga na kukarabati Mitaro ya mvua yenye urefu wa kilomita 4.76
ii) kuimarisha Maeneo ya Wazi kwa kufanya uboreshaji wa viwanja 3 vya mpira viliopo katika eneo la Sebleni Kwa Wazee
iii) Ujenzi wa barabara za ndani zenye urefu wa kilomita 9.14 na uwekaji wa taa zinazotumia nguvu za jua.
iv) kujenga soko moja la wajasiriamali katika eneo la Meya.
Aidha Katibu Mkuu ameweka saini kupitia Mradi wa Ukuzaji Uchumi Jumuishi Zanzibar ( BIG – Z) ambapo ni Mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Mradi utatekelezwa kwa miezi 30 Sawa na miaka 2 na nusu kuanzia tarehe ya leo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango
![](https://mofzanzibar.go.tz/newpofp/wp-content/uploads/2024/05/WhatsApp-Image-2024-05-03-at-17.42.25_2fd2cb76.jpg)
![](https://mofzanzibar.go.tz/newpofp/wp-content/uploads/2024/05/WhatsApp-Image-2024-05-03-at-17.42.42_a2dd19cb.jpg)