IMG-20240222-WA0023

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amefanya ziara ya kushtukiza katika Kampuni ya “Fanikisha Limited” iliyopo mpendae inayojishughulisha na Utoaji wa Huduma za Fedha.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Saada amegundua kuwa kampuni ya “Fanikisha Limited” ilikuwa inatoa huduma hizo bila ya kuwa na kibali kutoka Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango, ambapo ni kunyume kwa mujibu wa Sheria na Miongozo iliyoweka na Ofisi.

Kampuni ya “Fanikisha Limited” inatoza kiwango cha riba ya mikopo cha asilimia kumi na tano (15%) kwa mwezi badala ya kiwango cha asilimia tatu nukta tano (3.5%) kilichowekwa na Ofisi. Hata hivyo, mikopo iliyokuwa inatolewa na Kampuni ya “Fanikisha Limited” ni Mikopo Kaushadamu.

Hivyo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amechukuwa hatua ya kuifungia kampuni “Fanikisha Limited” Kutoa Huduma za Fedha nchini kuanzia tarehe 21 Febrauari, 2024 mpaka itakapokamilisha taratibu za Sheria na Miongozo iliyowekwa na Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

Aidha, Mhe. Dkt. Saada katika ziara hiyo ameongozana na Kamishna wa Sera za Kodi na Fedha wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango. Ng. Haji A. Haji

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango

Tags: No tags

Comments are closed.