Kitengo hiki kinahusika na kutoa huduma za ushauri wa masuala ya kisheria katika masuala mbali mbali yanayohusiana na majukumu ya Ofisi.Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.

Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria

  • Kutoa ushauri na msaada wa masuala ya kisheria katika Ofisi ya Rais Fedha na Mipango; 
  • Kutoa tafsiri za Sheria, Kanuni, Miongozo na mikataba mbalimbali kwa Ofisi, Idara/Taasisi na vitengo vya Ofisi;
  • Kuweka na kuhifadhi Kumbukumbu na majalada ya kesi za madai zinazohusiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
  • Kutoa msaada wa kitaalamu wakati wa maandalizi au uhuishaji wa rasimu mbalimbali za kisheria na kuwasilisha rasimu hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Wizara inayohusiana na masuala ya Sheria kwa hatua zaidi;
  • Kushiriki majadiliano mbalimbali yanayohusu sekta kuingia katika makubaliano au mikataba maalumu ya Ofisi/kisekta;
  • Kutunza na kuhifadhi nyaraka zote za kisheria na mikataba inayohusu majukumu ya Ofisi ya Rais Fedha na Mipango;
  • Kuchambua na kutafsiri sheria za sekta na kutoa ushauri wa kisheria;
  • Kupitia na kupendekeza marekebisho ya sheria za zinazohusiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.