Divisheni hii inahusika na shughuli za uandaaji na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoandaliwa na Ofisi ili kuhakikisha zinakwenda sambamba na malengo yaliyokusudiwa. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

Majukumu ya Divisheni ya Maendeleo ya Sera

  • Kutayarisha karatasi ya dhamira (concept paper) ya Sera zinazohitajika na kushauri kwa Uongozi wa Ofisi;
  • Kuchambua Sera zilizopo za Ofisi Kiuchumi, Kijamii na Kiutawala kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya utekelezaji;
  • Kuwasiliana na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango wakati wa kutayarisha na kutekeleza Sera mpya ili kuhakikisha kuwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya Kitaifa ikiwemo MKUZA II, Dira ya 2020 pamoja na Mipango Mikakati ya Ofisi, Maidara na Taasisi za Serikali.