Divisheni ya fedha na deni la Taifa inashughulika na udhibiti na usimamizi wa deni la Taifa.

Majukumu ya Divisheni ya Fedha na Deni la Taifa

  • Kusimamia Deni la Taifa kwa kuandaa muundo wa usimamizi wa deni na kuhakikisha mzigo wa madeni unadhibitiwa.
  • Kutathmini mapendekezo ya mikopo ya ndani na nje na kuandaa usimamizi wa kujitegemea katika wajibu wa kifedha wa Serikali.
  • Kudumisha “database” ya usimamizi wa madeni ya mikopo na dhamana ya Serikali.
  • Kuandaa ripoti za madeni kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma.
  • Kusawazisha taarifa za madeni ya Serikali na wanaotudai, BOT, Wizara ya Fedha na Mipango, SMT na wadau wengineo.
  • Kukusanya, kuhakiki na kutoa taarifa ya madeni yote ya ndani ya Serikali.
  • Kutayarisha makisio ya riba ya Deni la Umma na malipo ya Kima kwa ajili ya kuiingiza katika bajeti ya mwanzo.  
  • Kutimiza matakwa ya Serikali kifedha na kuweka gharama ndogo na madeni kadiri iwezekavo zinazohusiana na vihatarishi.
  • Kutunza kumbukumbu za Madeni ya Serikali na kufuatilia mfumo wa Usimamizi wa madeni.
  • Kutoa dhamana na kuweka kumbukumbu za malipo ya dharura kwa Taasisi za Umma, mashirika na Serikali za mitaa.
  • Kutoa taarifa za mwenendo wa Fedha katika Mfuko Mkuu, malipo ya deni na salio la mtawanyo wa mkopo.
  • Kutoa kazi za sekriterieti ya Kamati ya Usimamizi wa Deni la Zanzibar.