MUUNDO UNAOPENDEKEZWA WA OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO

Muundo wa sasa wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango unaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango. Katika ngazi ya kiutendaji Wizara inaongozwa na Katibu Mkuu akisaidiwa na manaibu makatibu wakuu wawili (2), Idara nane (8), Ofisi Kuu Pemba na Vitengo sita (6).  Aidha, Wizara ina jumla ya Taasisi nane (8) zinazojitegemea ambazo zipo chini ya Wizara hii, mchanganuo wa Idara, Ofisi Kuu Pemba, Vitengo na Taasisi Zinazojitegemea ni kama ifuatavyo: –