Divisheni hii inashughulika na uandaaji wa bajeti kwa kuingizwa taarifa za bajeti kwenye mfumo wa kielektronik.

Majukumu ya Divisheni ya Uandaaji Bajeti

  • Kuratibu uwasilishwaji wa bajeti za Mawizara na kusimamia uingizwaji wa taarifa za bajeti kwenye mfumo wa kielectroniki;
  • Kusimamia uchapishaji wa hutuba ya bajeti ya Serikali pamoja na makadirio ya Mapato na matumizi;
  • Kuratibu mswada wa fedha na matumizi;
  • Kuratibu utekelezaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Ofisi ya Mhasibu Mkuu/ Hazina, Idara ya fedha za nje na Tume ya Mipango;
  • Kubuni njia bora za kuandaa mijadala ya kibajeti inayohusiana na Mapato na matumizi kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
  • Kubuni makadirio na makisio ya Mapato na matumizi ya Serikali kwa Wizara na Taasisi za Serikali;
  • Kusimamia muongozo wa utayarishaji wabajeti;
  • Kuwasilisha nyaraka za bajeti kwa Makatibu Wakuu, Baraza la Mapinduzi (BLM) na Baraza la Wawakilishi (BLW);
  • Kubuni mipango kazi wa Idara kwa mashirikiano na divisheni nyengine;
  • Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.