Divisheni hii inashughulikia usimamizi wa mfumo wa matumizi ya Serikali pamoja na malipo ya Serikali.

Majukumu ya Divisheni ya Usimamizi wa Mfumo – IFMS

  • Kuhakikisha kuwa Mfumo wa Matumizi ya Serikali unafanya kazi kwa ufanisi na udhibiti mzuri na unawawezesha watumiaji wote wa mfumo katika kufanya kazi zao za kila siku na kuweza kutatua kasoro zinazojitokeza katika utendeaji.
  • Kusaidia uandaji wa taarifa za kifedha kwa watumiaji na kuhakikisha kuwa taarifa zote ziko sahihi.
  • Kusaidia ufungaji wa Hesabu za mwaka, kufanya usimamizi wa usanidi “configuaratuion” wa mfumo kwa kasma mpya na kuhamisha taarifa za bajeti kwenye mfumo.
  • Kuwasimamia watumiaji wa mfumo kapata haki za utumiaji, kuweka usalama mzuri kulingana na sera na taratibu za usalama na kufanya mapitio ya utaratibu uliopo na kusaidia kupata taarifa zilizopita, za ndani na nje kwa kuzingatia uhalisia.    
  • Kutekeleza mifumo bora ya usalama na vifaa katika majengo ya mfumo yaliyoko Unguja na Pemba na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kwa mujibu wa sera na taratibu za usalama.
  • Kupanga, kusimamia, kudhibiti, kuelekeza na kutathmimi utendaji wa taarifa za kieletroniki. 
  • Kufanya utafiti kwa ajili ya kugundua changamoto na vihatarishi vinavotokea katika utumiaji wa mfumo na kutafuta suluhisho na miongozo katika kutatua changamoto na vihatarishi hivyo.