Idara hii itashughulikia na uandaaji wa mipango ya Ofisi, bajeti, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za Ofisi na programu za miradi, kutayarisha na kuzifanyia mapitio Sera na kufanya tafiti za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Sera na Utafiti

  • Kuandaa Mpango wa Mwaka na Mpango Mkakati wa maendeleo wa muda wa Kati wa Ofisi;
  • Kufuatilia, kukusanya na kuratibu Mipango ya Maendeleo ya Taasisi;
  • Kuhakikisha kuwa rasilimali na fedha za Misaada inatumika vizuri;
  • Kutoa utaalamu na huduma kwa ajili ya Maandalizi, Mapitio, Ufuatiliaji na Sera mbalimbali za Sekta;
  • Kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji (disseminate) wa Takwimu mbalimbali za Ofisi kwa kushirikiana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali;
  •  Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango kazi na mpango wa matumizi wa Ofisi,
  • Kufanya ufatiliaji na tathmini wa utekelezaji mpango kazi wa Ofisi;
  • Kusimamia, kufanya mapitio na tathmini ya Sera, Mipango, Programu na Miradi mbali mbali ya Ofisi
  • Kuratibu shughuli za tafiti na kutayarisha maelezo ya kisera kutokana na tafiti hizo
  • Kuandaa bajeti ya Ofisi.

IMG_3169