Divisheni hii itahusika na shughuli za ufatiliaji na ufanyaji wa tathimini wa mipango mbali mbali ya Ofisi iliyopangwa kutekelezwa. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.

Majukumu ya Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini

  • Kuandaa Viashiria vya taarifa ya ufuatiliaji kwa kuzingatia mahitaji ya Mpango Mkuu wa Ufuatiliaji wa MKUZA;
  • Kutayarisha Mfumo na Muundo wa ukusanyaji wa Taarifa na Ripoti za utekelezaji;
  • Kuandaa na kushiriki ziara za Ufuatiliaji na Tathmini zinazofanyika na kuhakikisha zinafuata Mifumo iliyokubalika katika ukusanyaji wa taarifa ili ziweze kusaidia katika kutoa maamuzi ya Uongozi;
  • Kuanzisha Mfumo bora wa kukusanya matokeo ya Tathmini na Ufuatiliaji;
  • Kufuatilia utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Ofisi;
  • Kutayarisha Ripoti za utekelezaji wa majukumu ya Ofisi za robo mwaka, nusu, na mwaka
  • Kukusanya taarifa za uchambuzi wa Takwimu/Taarifa zinazohitajika katika kutayarisha Sera, Mipango pamoja na mapendekezo ya bajeti;
  • Kushiriki katika kutayarisha Mipango, Programu na shughuli za bajeti za Ofisi ikiwemo kutayarisha Malengo halisi ya utekelezaji na Viashiria;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwemo kuanzisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya Ofisi;
  • Kushirikiana na Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini cha MKUZA katika kutoa na kupokea taarifa za uhakiki katika kutayarisha Ripoti ya Mwaka ya MKUZA, Ripoti ya MDGs na Mpango Kazi wa Ofisi.