Divisheni hii itakuwa itahusika na Usimamizi wa Mfuko Mkuu wa Serikali pamoja na uingizaji wa fedha kwa MaOfisi.

Majukumu ya Divisheni ya Usimamizi wa Fedha:

  • Kusimamia na kutunza Mfuko Mkuu wa Serikali kulingana na Katiba na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma Na. 12, 2016.
  • Kusimamia “Exchequer Release” na kutoa Fedha kwa, Idara na Taasisi za Serikali zinazopaswa kuingiziwa fedha kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinzohusika.   
  • Kuongoza utekelezaji wa taratibu za lazima za Kihasibu na miongozo yake.
  • Kuandaa na kuwasilisha Jumuisho la Hesabu za Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.                                
  • Kufanya usuluhishi wa Hesabu za mapato na ulinganisho wa mapato hayo kwa Mamlaka (Taasisi) za ukusanyaji wa mapoto ya Kodi.
  • Kushirikiana na Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kwa kuanzisha na kusimamia malimbikizo ya mapato yasiyo ya kodi.
  • Kukadiria mahitaji ya Fedha za Serikali na kuhakikisha kuwa Fedha za kutosha zinapatikana kukidhi matumizi ya lazima ya Serikali kwa muda uliowekwa.
  • Kuandaa uwasilishaji wa matarajio ya mapato na matumizi kwa Kamati ya Ukomo ya Serikali (Government Ceiling Committee).
  • Kuandaa usuluhishi wa Kibenki kwa Hesabu zote za Hazina ya Serikali (Forex and Local Accounts).
  • Kutayarisha taarifa zinazoonesha vifungu tofauti vya budget, Fedha iliyotengwa, hesabu na usimamizi wa kihasibu wa kila siku.  
  • Kudhibiti matumizi kwa kulinganisha na mapato na kuhakikisha uwepo wa ukwasi (Liquidity Position).
  • Kuanzisha na kuweka daftari linaloonesha faida/hasara za Amana za Serikali.