Divisheni hii ina jukumu la kusimamia sera za kifedha ambazo zitaambatana na malengo ya uchumi mkuu, kutoa ushauri juu ya mambo yanayohusiana na fedha za umma na sekta zingine za kifedha, kama benki, fedha ndogo ndogo, mfuko pensheni, kampuni za bima na masoko ya mitaji.

Majukumu ya Divisheni ya Usimamizi wa Sera za Fedha

  • Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa sekta ya benki katika maendeleo ya uchumi.
  • Kushauri, Serikali juu ya zana madhubuti za kuzuia matumizi mabaya ya mfumo wa kifedha, uhalifu wa kifedha pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.
  • Kushiriki na kushauri juu ya mikutano ya kitaifa, kikanda nakimataifa juu ya maendeleo ya sekta ya benki
  • Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sekta ya Bima na Masoko ya Mitaji, katika maendeleo ya uchumi.
  • Kuchukua hatua sahihi katika kuboresha uimara wa kifedha na sekta isiyo ya benki.
  • Kuratibu utaratibu wa utoaji wa mikopo na masoko ya hisa kwa kufadhili shughuli za biashara na uwekezaji wa muda mrefu.
  • Kuunda uratibu mzuri, udhibiti na usimamizi wa sekta ndogo ndogo za kifedha.
  • Kukuza utafiti, ubunifu na maendeleo ya huduma za taasisi ndogo ndogo za kifedha zinayohusisha usalama mzuri kwa watumiaji ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi, ajira na kupunguza umaskini
  • Kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ndogo ndogo ya fedha.
  • ii)     Ofisi Kuu – Pemba

Ofisi hii itahusika na jukumu la uratibu na usimamia shughuli za Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba. Ofisi itaongozwa na Ofisa Mdhamini atakaeteuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.  Aidha, Ofisi Kuu Pemba itakuwa na divisheni ambazo zinawakilisha utekelezaji wa majukumu mbali mbali yaliyomo katika Idara za Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.

2.5 VITENGO

Majukumu ya Vitengo sita (6) vilivyo chini ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ni kama ifuatavyo: