IMG-20240718-WA0023

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Mashirikiano ya Kimataifa la Korea (KOICA)

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Mashirikiano ya Kimataifa la Korea (KOICA) Mkurugenzi Manshik Shin na Ujumbe wake katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango Mazungumzo hayo yamelenga katika kuimarisha mashirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Korea Kusini kupitia Shirika Hilo. Kikao hicho kilihudhuriwa na Sekta mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwemo Sekta ya Utalii, Elimu, Uchumi wa Buluu, Kilimo, Uwekezaji na Biashara.

Dkt. Juma Malik amemuhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Zanzibar ipo tayari kushirikiana na Korea katika kuimarisha mashirikiano yaliyopo ili kuweza kutatua changamoto.

Dkt. Juma amemesema kuwa Zanzibar imewasilisha maandiko ya Miradi 15 kwa mazingatio ya kupatiwa ufadhili kutoka katika Shirika hilo la KOICA na miradi hiyo ina lengo la kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (ZADEP) ili kuweza kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar.

Nae, Mkurugenzi Manshik Shin aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ambayo imekuwa ikiipatia Korea katika kuimarisha mahusiano baina ya Korea na Zanzibar. Mkurugenzi huyo aliahidi kufanyia kazi maeneo ambayo yamewasilishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kuyapatia ufadhili na ameahidi kushirikiana na Sekta mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha mashirikiano ili kuleta maendeleo na mafanikio Nchini.

Mkurugenzi Manshik ameahidi kuyafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa katika kikao hicho ikiwemo kuisaidia Zanzibar katika kuipatia ufadhili wa Elimu ya Juu kwa wafanyakazi wa Serikali ikiwemo Shahada ya Uzamili na Uzamivu, Kuimarisha mashirikiano ya Kisekta, Kuichangia mfuko wa Ufadhili wa Sekta ya Afya Pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango alisositiza kwa kuliomba Shirika hilo kuendelea kuisaidia Zanzibar na kuzingatia maombi ambayo yamewasilishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Sekta mbalimbali na kuahidi kuwa milango ya Zanzibar ipo wazi wakati wote kuhakikisha inaimarisha mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango

WhatsApp Image 2024-05-03 at 17.42.26_78525633

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini na kampuni ya CRJE juu ya Mkataba wa Ujenzi Mradi wa Uimarishaji wa Miji Kwa Upande wa Unguja.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo tarehe 2/05/2024 imetiliana saini na kampuni ya CRJE juu ya Mkataba wa Ujenzi Mradi wa Uimarishaji wa Miji Kwa Upande wa Unguja.

Kwa niaba ya Serikali Mkataba huo umewekwa saini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil ambapo jumla Bilioni 40,535,043,304.24 zinatarajiwa kutumika kwa ujenzi wa maeneo ya Sebleni – Kwa Wazee, Meya- Magomeni na Mtaro wa Mfumo C, kwa upande wa CRJE mkaba huo umesainiwa na XU Chang ambae ni Meneja wa kampuni.

Mradi huo utaipa hadhi na kuyakuza maeneo ya Mjini kwa i ) kujenga na kukarabati Mitaro ya mvua yenye urefu wa kilomita 4.76
ii) kuimarisha Maeneo ya Wazi kwa kufanya uboreshaji wa viwanja 3 vya mpira viliopo katika eneo la Sebleni Kwa Wazee

iii) Ujenzi wa barabara za ndani zenye urefu wa kilomita 9.14 na uwekaji wa taa zinazotumia nguvu za jua.

iv) kujenga soko moja la wajasiriamali katika eneo la Meya.

Aidha Katibu Mkuu ameweka saini kupitia Mradi wa Ukuzaji Uchumi Jumuishi Zanzibar ( BIG – Z) ambapo ni Mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Mradi utatekelezwa kwa miezi 30 Sawa na miaka 2 na nusu kuanzia tarehe ya leo.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango

katibu2

Katibu Mkuu Dkt. Juma Malik Akil leo akutana na Ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC)

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil leo tarehe 30/04/2024 amekutana na Ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) ambao wapo Zanzibar kwa ziara ya kimasomo. Katibu Mkuu Dkt. Juma amesema ziara hii ina mwanya wa kiuchumi na kiutamaduni na Zanzibar inaendelea kujenga miundo mbinu wezeshi kwa uchumi wa buluu. Dkt. Juma amesema Ujio huu ni kundi la 12 kuja kuitembelea Sekta ya Fedha ambayo ni sekta muhimu inayosimamia Uchumi wa Nchi. Ujumbe huo unajumuisha wanafunzi wa Nchi 15 za Dunia ikiwemo Tanzania. Aidha, Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango imepata nafasi ya kuelezea kazi inazozifanya kupitia Taasisi zake ikiwemo Tume ya Mipango, PBZ, ZRA, TRA, ZIAT na Ofisi ya TR. Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi cha Taifa Balozi Meja Generali Wilbert Augustine Ibuge. kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Bima wa Zanzibar(ZIC).

IMG-20240222-WA0023

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amefanya ziara ya kushtukiza katika Kampuni ya “Fanikisha Limited” iliyopo mpendae inayojishughulisha na Utoaji wa Huduma za Fedha.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Saada amegundua kuwa kampuni ya “Fanikisha Limited” ilikuwa inatoa huduma hizo bila ya kuwa na kibali kutoka Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango, ambapo ni kunyume kwa mujibu wa Sheria na Miongozo iliyoweka na Ofisi.

Kampuni ya “Fanikisha Limited” inatoza kiwango cha riba ya mikopo cha asilimia kumi na tano (15%) kwa mwezi badala ya kiwango cha asilimia tatu nukta tano (3.5%) kilichowekwa na Ofisi. Hata hivyo, mikopo iliyokuwa inatolewa na Kampuni ya “Fanikisha Limited” ni Mikopo Kaushadamu.

Hivyo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amechukuwa hatua ya kuifungia kampuni “Fanikisha Limited” Kutoa Huduma za Fedha nchini kuanzia tarehe 21 Febrauari, 2024 mpaka itakapokamilisha taratibu za Sheria na Miongozo iliyowekwa na Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

Aidha, Mhe. Dkt. Saada katika ziara hiyo ameongozana na Kamishna wa Sera za Kodi na Fedha wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango. Ng. Haji A. Haji

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango

IMG-20240212-WA0029

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum kuongoza kikao cha Uongozi.

Kikao hicho kimejadili agenda mbalimbali za kimaendeleo kikao hicho pia kimepata fursa ya kumuaga aliekuwa Naibu Waziri Mhe. Ali Suleman Ameir ambae amepata uteuzi na kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Ikulu.

Kikao hicho pia kimepata fursa ya kumkaribisha Naibu Waziri Mhe. Juma Makungu Juma na kuendelea kujadili mada mbalimbali zilizowashilishwa katika kikao hizho cha Uongozi wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

WhatsApp Image 2024-01-23 at 08.54.33_51d33f48

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum ameendesha kikao cha Jukwaa la Uchumi na Bajeti kwa upande wa Serikali kuu kwa mujibu wa sheria ya Fedha.

Mhe Dkt Saada Mkuya Salum amewataka wanasheria wote wa serikali na makatibu wakuu kuacha kusaini mkataba wowote wenye vipengele vya kodi na baadae kuomba kusamehewa kodi kwani hiyo sio kazi yao kwani msamaha wa kodi unatolewa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango na msamaha unautaratibu wake ambao upo kisheria .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza hayo wakati akifungua Jukwaa la bajeti la mwaka 2024/2025 kwa serikali kuu liloshirikisha makatibu wakuu katika ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni.

“Tufahamu kuwa kodi inayokusanya ndio sisi inayotulipa mishahara, huduma za afya, elimu na huduma nyengine za barabara, maji, pencheni zinatokana na hii kodi,” alisema.

Hivyo, aliahidi kwamba Ofisi yake itaendelea kulisimamia jambo hilo ili kuona kunakuwa na nidhamu ya ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuangalia namna bora ya kuhakikisha kila mmoja anawajibika katika usimamizi wa sheria za kodi nchini.

“Jambo hili tutaendelea kulisisitiza ili kufikia utekelezaji wa bajeti kwa zaidi ya asilimia 100 na jambo hili linawezekana ikiwa kila mmoja wetu atakuwa mlinzi wa kodi ambazo ni fedha za umma,” alisisitiza.

Waziri Saada akizungumzia bajeti zinazotaarishwa kuzingatia masuala ya kijinsia alisema bado kuna muamko mdogo kuhusiana na utayarishaji wa bajeti unaozingatia jinsia hasa kunufaika kwa wanawake katika masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, afya na mambo mengine.

Alisema pamoja na kujaribu kujenga uwezo kwa watendaji lakini jambo hilo bado halijafanikiwa hivyo Ofisi yake itahakikisha inaweka nguvu kubwa katika baadhi ya wizara tano ikiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Elimu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Wizara ya Uchumi wa Bluu ili kuona namna gani wataweza kutekeleza bajeti zinazozingatia jinsia.

Mbali na hayo Waziri Saada alisema wizara italifanyia kazi eneo la manunuzi na eneo la mapato ili kuhakikisha manunuzi yote yanayofanywa serikalini yanazingatia sheria.

“Mara hii tunakwenda kwenye bajeti ambayo ya uhalisia utaingiziwa fedha na kazi zako utaonesha unazotakiwa uzifanye kisingizio cha kuwa huna pesa hujafanya hicho kitakuwa kimeisha.

Jukwa hilo limehudhuriwa na Viongozi wakuu wa Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

Aidha, washiriki wa jukwaa hilo walimuomba Mwenyekiti kuzingatia mijadala yao
Sambamba na hayo walisisitiza kuomba kuwa miradi ya kimkakati kusimamiwa na serikali kuu na sio Idara au Mashirika ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati.

Jukwaa hilo lipo kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa fedha za umma ambapo mada mbalimbali za uchumi na matumizi ziliwasilishwa na kuzingatia matumizi na makusanyo ya bajeti kwa mwaka 2024/2025.

WhatsApp Image 2023-11-06 at 11.58.47

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya afungua kongamano la Miaka 3 ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Novemba 5,2023 alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kuadhimisha miaka mitatu (3) ya Uongozi wa Rais WA Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi

Kongamano hilo limetayarishwa na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango pamoja na taasisi zake ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu mbali mbali walialikwa katika kongamano hilo, miongoni mwa Vyuo Vikuu vilivyoshiriki ni pamoja na Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA), Chuo Cha Utawala WA Umma(IPA), Chuo Cha Mwalimu Nyerere, Zanzibar University (ZU) pamoja na Al Sumeit Cha Chukwani

Lengo la kongamano hilo ni kuyaelezea Mafanikio ya Miaka mitatu (3) ya Dkt Mwinyi Madarakani

Katika Kongamano hilo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil aliwasilisha Ripoti ya utekelezaji ya Miaka mitatu ya Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na kueleza kuwa Miaka mitatu Dkt Mwinyi Miradi mbalimbali ya Maendeleo imetekelezwa, Miradi ya Skuli, Hospitali, Barbara, Bandari na kuongeza pencheni jamii kutoka 20,000/ Hadi 50,000/ pamoja na nyongeza ya mishahara

Aidha, taasisi za ofisi ya Rais Fedha na Mipango zilipata fursa za kuwasilisha taarifa zao za utekelezaji wa Miaka mitatu, taasisi zilizowasilisha taarifa zao ni Shirika la Bima la Zanzibar, Benkj ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Mamlaka ya Manunuzi pamoja na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA)

Nao, baadhi ya wanafunzi walipata fursa ya kuelezea Mafanikio ya Dkt. Mwinyi, Ali Ahmada kutoka Chuo Kikuu Cha Summeit Chukwani ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kwa kazi kubwa wanayoifanya kuleta Maendeleo na kuiomba Serikali kuongeza kiwago Cha Fedha za mikopo Kwa wanafunzi WA vyuo vikuu

Aisha Mussa kutoka Chuo Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) ameitaka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango kuwapatia elimu na mafunzo wajasiriamali juu ya matumizi ya Mifumo ya kidigitali katika kazi zao

Imetolewa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mioango.

WhatsApp Image 2023-11-06 at 11.51.51 (1)

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya azindua Bodi ya ZIAAT

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Novemba 3,2023 amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi (ZIAAT) katika Ukumbi wa taasisi hiyo uliopo katika jengo la iliyokuwa Ofisi ya Mfuko wa Barabara Maisara Mjini Zanzibar

Mhe. Waziri amewataka wajumbe wa Bodi hiyo wawe wabunifu na wasimamie taasisi Kwa maslahi ya Umma pamoja na kufanya uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt. Saada ameshauri kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa (ZIAAT) wapitie vizuri Sheria ya (ZIAAT) na wafanye maboresho ya kuingiza masuala ya miamala ya fedha katika Sheria za kiislam pamoja na mambo mengine

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Bw. Juma Amour Mohammed ameeleza kuwa Bodi itafanya kazi Kwa uweledi wa hali ya juu katika kuboresha tasnia ya uhasibu na Ukaguzi pamoja na kutoa elimu Kwa wajumbe wa Bodi ili wafahamu Sheria ya (ZIAAT)

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi CPA. Ame Burhan Shazil ameeleza kuwa taasisi hii imeanzishwa Kwa Sheria No 7 ya Mwaka 2022 malengo yake ni pamoja na kuongeza ubora wa huduma zitolewazo na (ZIAAT), kuwatambua na kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa kodi

Katika hafla hiyo, pia alikuwepo Muwakilishi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi CPA Charles Masabu ambae ameitaka (ZIAAT) kufanya kazi zake kitaalamu zaidi na wakianza tu kuwasajili Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi ni vyema wakasajiliwa Kwa njjia ya kieletroniki na hili litarahisisha ukusanyaji wa Kodi

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha n Mipango

WhatsApp Image 2023-10-27 at 14.39.41

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya akutana na Uongozi wa ASA Microfinance Limited

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Oktoba 26, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kifedha (ASA Microfinance Limited) Bibi Karin A. M.Kersten) ambae ameambatana na wajumbe mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa ASA Kwa upande wa Tanzania Ndg Muhammad Shah Newaj

Bibi Kersten ameeleza kuwa Uongozi wa ASA umefika Ofisini Kwa Mhe. Waziri Kwa lengo la kujitambulisha na kueleza kuwa Kwa upande wa Tanzania Ofisi za ASA Microfinance Limited zinapatikana Kinondoni, Jijini Dar es Salaam

Aidha, Bibi Kersten ameendelea kueleza kuwa Kwa upande wa Zanzibar Ofisi za ASA zinapatikana Maungani, Wilaya ya Magharib ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharib

Dkt Saada Mkuya ameushukuru Uongozi wa ASA Kwa kufungua tawi lake Kwa upande wa Zanzibar kwani itakuwa ni fursa Kwa wajasiriamali wa sekta mbalimbali hasa sekta ya Uchumi wa Buluu kwani ndio kipaumbele Cha kuwakomboa Wazanzibari wengi ambao wanajishhhulisha na kilimo Cha mwani na uvuvi wa kawaida.

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango

WhatsApp Image 2023-10-26 at 08.10.41

Dkt Saada amuwakilisha Mhe. Rais katika Uzinduzi wa Airpay Tanzania na PPP Portal

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Oktoba 25, 2023 amemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Uzinduzi wa Airpay Tanzania pamoja na mfumo wa Public Private Partnership (PPP) katika Ukumbi wa Golden Tulip Mjini Zanzibar

Mhe. Saada Mkuya Kwa niaba ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa zana ya Uchumi wa Buluu itafanya kazi vizuri kupitia mfumo wa Airpay kwani itarahisisha miamala ya kifedha Kwa njia za cashless pamoja na kuweza kutambua miamala ya kifedha inayofanywa na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta hiyo.

Mhe. Waziri Saada ameitaka Airpay Tanzania kufanya kazi Kwa karibu na Taasisi za SMZ kama ZRA ili kurahisha ukusanyaji wa Kodi Kwa njia za kieletroniki

Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Airpay Mr Kunal Jhunjhunwala ameeleza kuwa lengo la teknolojia hii ni kurahisisha miamala ya kifedha na malipo na Kila mtu aweze kufikiwa na kutumia huduma hii

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Ndg Said Seif Said ameeleza kuwa Airpay Tanzania itasaidia Wananchi kupata huduma Kwa njia ya kidigitali pamoja na kuwarahisishia wawekezaji na wafanyabiashara kujisajili na kufanya malipo Kwa urahisi zaidi

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango